RAIS MAGUFULI AMTEUA NA KUMUAPISHA KAMISHNA DIWANI ATHUMAN KUWA MKURUGENZI MKUU USALAMA WA TAIFA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 12 September 2019

RAIS MAGUFULI AMTEUA NA KUMUAPISHA KAMISHNA DIWANI ATHUMAN KUWA MKURUGENZI MKUU USALAMA WA TAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani Msuya Kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (DGIS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 12, 2019.

RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua na kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Uteuzi wa Kamishna Diwani Athuman Msuya umeanza leo tarehe 12 Septemba, 2019 na ameapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani Athuman Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Akizungumza baada ya kumuapisha, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Kamishna Diwani Athuman Msuya kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Kamishna Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.

No comments:

Post a Comment