| Elimu ya sayansi ya hali ya hewa ikiendelea kutolewa - Simiyu. |
Katika ufunguzi wa maonesho hayo tarehe 01 Agosti 2019, Mhe. Samia aliwataka watafiti wote nchini kutoa matokeo ya utafiti kwa walengwa kwa kuwapatia elimu ya kutosha ili waweze kunufaika na tafiti hizo.
“Nitoe rai kwa watafiti wote nchini kutoa matokeo ya tafiti zenu kwa walengwa na kuwapa elimu ya kutosha ili waweze kunufaika ipasavyo” aliongea mama Samia.
Katika kufanikisha rai hiyo ya Makamu wa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, TMA imeanza kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya umuhimu wa kutumia taarifa za hali ya hewa katika kufanya shughuli zao zenye kuleta tija hususani wakulima na wavuvi ambapo zoezi la utoaji wa elimu hiyo linatarajiwa kuendelea mpaka siku ya kilele cha maadhimisho hayo tarehe 08 Agosti 2019.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


No comments:
Post a Comment