Mkurugenzi wa M-Commerce Vodacom Tanzania, Epimarck Mbeteni (kulia) akishikana mkono na Kamishna wa Vibali, Mary Palmer, kuashiria uzinduzi wa huduma ya ‘Malipo ya Uhamiaji kwa M-Pesa’ wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika makao ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom sasa wanaweza kufanya malipo ya huduma za Uhamiaji moja kwa moja kupitia menu ya M-Pesa na Vodacom App. |
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania Plc kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini wamezindua huduma
mpya iitwayo ‘Malipo ya Pasipoti kwa M-Pesa’ katika hafla fupi iliyofanyika
ofisi za makao makuu ya Uhamiaji, kurasini, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo
Mkurugenzi wa M-Commerce, Epimack Mbeteni alisema huduma hii mpya inalenga
kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kufanya malipo kwa haraka na urahisi zaidi.
“Napenda kuwataarifu wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kwamba, sasa wanaweza
kulipia hati zao uhamiaji kwa kupitia M-Pesa”.
“Ili mteja aweze kulipia inabidi
aingie kwenye menu ya M-Pesa na kufuata utaratibu wa kulipa malipo ya serikali
au kupitia zana (app) M-Pesa. Lengo letu ni kuhamasisha Watanzania wapate hati
mpya za kieletroniki lakini pia kuwasogezea huduma za malipo viganjani kwao,
ndio maana tumeona umuhimu wa kushirikiana na Uhamiaji kufanikisha hili”
Aliongeza Mbeteni.
Huu
ni mkakati wa kuwarahishia waombaji wa hati za kusafiria (Passport) ulipaji wa
malipo kwa idara ya Uhamiaji, kwa vile walikuwa wakipanga foleni na kusubiria
kwa muda mrefu ili kukamilisha malipo hayo.
Kamishna
wa Passport wa Uhamiaji Marry Palmer alisema “tuna furaha
kuungana na Vodacom Tanzania Plc kuwawezesha wateja kufanya malipo kirahisi,
vile vile kuiwezesha idara yetu kufanya kazi kwa urahisi zaidi. Nategemea kuona
bunifu nyingi zaidi kutoka Vodacom”.
Vodacom
imedhamiria kufikia idadi kubwa ya watu ambao hawapo kwenye mifumo rasmi ya
kifedha, kuchochea ujumuishwaji, na uwezeshaji kupitia huduma rafiki na salama
hivyo hii ni moja ya njia ya kufanikisha lengo hilo.
“Tunaendeleza nia ya kubadili Tanzania
kuwa jamii inayofanya malipo kidijitali, tunawekezakatika teknolojia ya simu
ambayo itaingiza watu wengi zaidi katika mifumo ya kifedha nahatimaye, kufikia
malengo ya kijamii na kiuchumi ya nchi”, alisisitiza mbeteni.
Kampuni ya Vodacom imedhamiria
kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali ikiwa ni pamoja na kukuza
matumizi ya pesa mtandao (E-money) kupitia mtandao wake ulioshamiri nchi nzima
ambayo itasaidia wananchi kuepuka hatari mbalimbali zitokanazo na kubeba fedha
kila wanapotaka kufanya manunuzi.
No comments:
Post a Comment