Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wakati akiwataka viongozi wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kukigawa chama na kufifisha juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuleta maendeleo kwa wananchi kama anavyokusudia.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi. |
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
MKUU wa mkoa wa Iringa Ally
Hapi amewataka viongozi wastaafu wa chama cha mapinduzi kuacha kukigawa chama
na kufifisha juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuleta
maendeleo kwa wananchi kama anavyokusudia
Akizungumza na vyombo vya
habari ofisini kwake mkoani Iringa,Hapi alisema kuwa kumshambulia Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaishamburia na kuihujumu serikali yote.
“Unapomshambulia Rais
unatushambilia hadi sisi wakuu wa mkioa na wateule wote ambao ametuteua
kumsaidia kazi kwa kumuhujumu juu ya utendaji wake wa kazi kwa kuleta maendeleo
kwa wananchi” alisema Hapi
Hapi alisema kuwa Membe
hajaanza leo kumuhujumu Rais Magufuli kwa ajili bado anahasira za kukosa urais
kwa kuwa alikuwa amejipambanua kuwa alikuwa Rais mtarajiwa wakati wa uchaguzi
wa mwaka 2015.
“Membe anafurahi sana nchi
kupasuka vipande vinne kwenye clip yake kwa kusema ni aibu sana kumpata Rais
kama Magufuli anazungumza sana hiyo yote bado inamuuma kuukosa urais ambao
tayari alikuwa amejitangazia kuwa yeye ndio alikuwa anastahili kuwa Rais”
alisema Hapi
Aidha Hapi alisema kuwa mzee
Membe amekuwa akilalama kuwa Rais magufuli kuwateuwa viongozi walikuwa
wapinzani kuongoza taifa katika nyadhifa mbalimbali tofauti na utamaduni wa
chama hicho ulivyokuwa hapo awali.
“Mbona hakusema kwenye
serikali ya awamu ya Nne kwa Rais mstaafu Dr Jakaya Kikwete alipowateu
wapinzani kushika nafasi mbalimbali ambazo zilikuwa nyeti kwa wakati huo mbona
wote walikaa kimya kwanini leo hii iwe kwa Rais Magufuli” alisema Hapi
Lakini Hapi alisema kuwa
viongozi wanaomhujumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewahi kuwa
viongozi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vya taifa.
“Mzee Kinana alikuwa kanali
wa jeshi,mzee Makamba amekwenda kwenye vyuo mbalimbali vya jeshi na Membe
amefanya kazi kwenye idara nyeti za usalama wa taifa ni watu waliokula kiapo na
ni watu ambao usinge wategemea kumong’onyoa umoja na mshikamano na kuhatarisha
tunu ya taifa letu” alisema Hapi
Hapi amewatakwa wazee wa
chama cha mapinduzi kufuata utaratibu wa utawala huu na kutii mamlaka iliyopo
madarakani.
“Leo wazee wetu wamekwama
wapi hadi kuamua kuchua uwamuzi wa kuandika waraka na kuusambaza kwenye vyombo
mbalimbali vya habari katika jambo ambalo walikuwa wanaweza kuomba nafasi ya
kuonana na Rais ili kumueleza nini wanataka kuyaeleza” alisema Hapi
Hapi amemaliza kwa kulitaka
genge ambalo limekuwa likitengeneza njama za kumhujumu Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania waache mara moja kwa kuwa Rais Magufuli ni kipenzi cha
watanzania.
No comments:
Post a Comment