BENKI ya NMB imezindua tawi jipya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita
kwa lengo la kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja hivyo kusaidia
ukuaji wa uchumi katika kanda ya Magharibi. Hilo ni tawi la 25 kwa mkoani Geita
na la 229 nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua tawi hilo, mgeni rasmi
Mkuu wa mkoa wa Geita Eng. Gabriel Luhumba amesema ufunguzi wa tawi hilo
umekuja wakati muafaka kwa kuwa ofisi za serikali zinampango wa uchumi
wakimkakati ambao utafanya Geita kuwa chachu ya maendeleo nchini.
Akiongea na wananchi wa wilaya ya Mbogwe Eng. Gabriel Luhumba
pia ametoa rai kwa wananchi kubadilika na kuacha mazoea ya kuweka pesa
majumbani na kuwataka kuwa na tabia ya kuweka benki na kwenye taasisi za
fedha.
Eng.Luhumba alisema wananchi wa mkoa wa Geita wenye neema nyingi
ya madini aina ya dhahabu wamekuwa na tabia ya kutunza fedha zao
nyumbani hali ambayo imekuwa ni hatari kwa usalama wa maisha yao na kuwataka
kuacha tabia hiyo.
Alisema mazoea na tabia ya kuweka fedha kwenye
vitanda , kuchimbia chini au kwenye mazizi ya mifungo ilishapitwa na
wakati kwa kipindi
hiki na kuwataka vipato vyao
vya pesa wanapopata kwenda kuziweka benki na kwenye
taasisi za zinazotunza fedha.
“Ndugu zangu wananchi uhai katika maisha yetu ni bora
sana, katika familia zetu , tabia ya kuendelea kukaa na fedha
majumbani kwetu ni hatari sana kwa sababu unaweza kuvamiwa na watu
waharifu wakawashambulia na kupoteza maisha kwa
hiyo rai yangu mnapopata pesa iwe
hata kidogo lazima tupeleka kuziweka benki,, Alisema Eng.Luhumba.
Eng. Luhumba katika hotuba yake alitoa wito kwa wananchi wa
wilaya ya Mbogwe kutumia fursa zinazotolewa na benki hiyo kujiletea mafanikio
kiuchimi katika maisha yao na kuwataka kuwa wakopaji wazuri wa mikopo na
kulejesha kwa wakati.
Mbali na kuipongeza menejimenti ya benki hiyo, aliipa changamoto
ya kuhakikisha inaweza kuandaa Kongamano la biashara katika mkoa wa Geita
ilikuwapa msasa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu kuchangamkia
fursa zilipo mkoani humo ilikuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yenye tija
ndani na nje ya kanda ya Magharibi na Afrika Mashariki.
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi alisema anaishukuru
benki ya NMB kwa kuwasogezea huduma za kibenki kutokana na kuwa wananchi
walikuwa na kilio cha siku nyingi kwa serikali kuitaka benki kwa
sababu walikuwa wasafiri zaidi ya kilimita 50 kufaata huduma hizo wilaya jirani
za Bukombe na Kahama mkoa wa Shinyanga.
Mkupasi alisema kufunguliwa kwa tawi hilo la benki hiyo
kumewaondolea aza waliyokuwa wanaipata kusafiri na fedha umabari mrefu hali
iliyokuwa inahatarisha maisha yao kwa kuhofia kuvamiwa na majambazi
, kwa kusogezewa huduma hiyo na kuwahimiza kutumia fursa hiyo
kuichumi na kujiletea maendeleo.
Awali katika hotuba yake mkuu wa kitengo cha biashara wa benki
ya NMB , Donatus Richard alisema sasa tawi hilo ni la 229 kwa nchi
zima na huo ni wajibu wao katika kuwasogezea
huduma hizo wananchi, wafanyabiashara wa
dogo, wa kati na wakubwa ili kuwawezesha watu kupata mitaji kwa ajili ya
biashara na shughuli mbalimbali nalengo la kuwanyanyua kiuchumi na kuwaomba
wachangamikie fursa zionazotolewa na benki ili kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment