Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Fredy Mgunda wa kituo cha Radio Nuru FM Iringa ambaye amepata mafunzo kutoka Mradi wa Boresha Habari na kukiri kuwepo kwa kero hiyo inayotokana na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwa na uhaba wa magari ya kuondolea taka katika mitaa mbalimbali. |
Mmoja ya wanafunzi akipita katika kontena la kuhifadhia taka taka lilopo Manispaa ya Iringa ambalo wananchi wanalilamikia.
Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Fredy Mgunda wa kituo cha Radio Nuru FM Iringaambaye amepata mafunzo kutoka Mradi wa Boresha Habari akimuoneshea umbali wanakotoka wananchi kuja kutupa taka kwenye kontena hilo.
NA
FREDY MGUNDA, IRINGA
WANANCHI
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko
kutokana na Serikali kushindwa kuzoa taka kwa wakati katika makontena ya
kuhifadhia taka taka mbalimbali zilizopo katika maeneo ya halmashauri hiyo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi walisema makontena ya kuhifadhia taka taka yamekuwa
ni hatari kubwa hasa kwa watoto ambao wanacheza karibu na mazingira ya maeneo
hiyo hali inayopelekea kuhofia kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
“makontena
ya kuhifadhia taka taka haya ya kubebea taka taka yanatuathiri sana kutoka na
uchafu ulipo, unakuta wametupa Mbwa waliokufa, taka taka zilizooza ambazo ndio
zimekuwa zikisababisha magonjwa ya milipiko, hivyo tunaomba serikali iwe makini
na haya makontena ya taka taka,” walisema Wananchi.
Wananchi
hao walisema kuwa uongozi wa halmashauri umekuwa ukiwajibu wananchi kuwa tatizo
ni kukosekana kwa mafuta kwenye gari ambazo zimekuwa zikitumika kubebea makontena
ya kuhifadhia taka taka jambo ambalo limekuwa likiwakera wananchi kutokana na
kauli hiyo.
“Mwandishi
ukiwaambia viongozi kuhusu tatizo hili la kujazana kwa taka taka kwenye maeneo
haya ni kutokana na uongozi wetu wa halmashuri ya manispaa ya Iringa kusema
kuwa hawana mafuta,sasa sisi wananchi tunaoteseka tunakuwa hatuna cha kufanya”
walisema Wananchi
Aidha wananchi hao walisema kuwa maeneo
mengi ya kutupa taka taka hizo yanapakana na shule za misingi zilizopo katika
halmashauri ya manispaa ya Iringa hivyo inapelekea kuhatarisha afya za
wanafunzi wetu ambao bado ni watoto wadogo.
Hiki
kipindi cha vua na taka zinatupwa karibu kabisa na maeneo ambayo yanashule zetu
za msingi na watoto wetu wanapita katika maeneo hayo na wengine wapenda kucheza
katika maeneo hivyo ni hatari sana kwa watoto kupata magonjwa ya mlipuko”
walisema Wananchi
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada amekiri kuwepo kwa kero kwani inatokana na Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa kuwa na uhaba wa magari ya kuondolea taka katika mitaa mbalimbali.
“Niwaambie
ukweli hata mimi ni mmoja ya waathirika wa taka taka hizi ambapo naona hali hii
ikiendelea kuwa hivi basi yawezekana kukalipuka kwa magonjwa ya milipuko
kutokana nauchafu ulipo na sio kata hii hata kata zingine hali hii ipo kama
hapa” alisema Ngwada
Ngwada
alisema kuwa mikakati ni kuhakikisha anaibana halmashauri kuchukua uchafu huo uliopo kwenye makontena
ya kuhifadhia taka taka yanatolewa kwa wakati maana hakuna namna nyingine zaidi
ya hiyo.
“Sisi
hatuna uwezo wa kutoa hapa hizi taka taka kuzipeleka Kihesa Kilolo ambao ndio
kuna eneo la kutupa taka taka zote za halmashauri ya mji ,hivyo ni lazima
halmashuri iwajibike kwa jukumu la kutoa hizi taka taka kwa wakati ili
kuwaondolea kero wananchi wetu” alisema Ngwada.
Ngwada
aliupongeza Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa
mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika
la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa kuwapa mafunzo waandishi wa
habari na kusababisha kuibua kero za wananchi na kucha kuandika habari za
viongozi tu.
“Kwa
kweli mradi huu umenifurahi maana sijawahi kupata waandishi wengi wakija katika
kata yangu na kuibua kero za wananchi kama hivi bari hii ndio mara ya kwanza na
naomba waandishi wa radio Nuru fm endeleeni hivi hivi kwa kuwa mtatukumbusha
viongozi kuwatumika wananchi vilivyo” alisema Ngwada.
Katika
mafunzo hayo Mkufunzi kutoka Mradi
wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya
Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la
Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Temigunga Mahondo aliichagua habari
hii kutoka group na moja kuwa ndio habari iliyoandikwa kwa kiwango
kinachotakiwa kutokana na mafunzo.
Naye Afisa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Christian Ndenga amesema kuwa changamamoto
inayopelekea takataka kukaa muda mrefu kwenye makontena ya kuhifadhia taka taka
ya mitaa ni kutokana na mji kukua pamoja na kuharibika kwa magari ya kuzolea
taka.
Changamoto
kubwa ni kuharibika kwa magari yetu na magari mengine kwenda kufanyiwa
matengenezo ya kawaida hivyo kukosekana kwa gari moja tu kwa siku lazima
tutazidiwa tu kutoa taka taka hizo.
Licha
ya wananchi kulalamikia kuwepo kwa mrundikano wa taka kwa muda mrefu manispaa
ya Iringa hivi karibuni imeshika nafasi ya kwanza kati ya manispaa zote hapa
nchini kwa usafi.
No comments:
Post a Comment