WANAKIJIJI KITANDI WAMLILIA DC KUKEMEA DAWA ZA UZAZI WA MPANGO KWA WANAFUNZI WA MSINGI NA SEKONDARI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 7 April 2019

WANAKIJIJI KITANDI WAMLILIA DC KUKEMEA DAWA ZA UZAZI WA MPANGO KWA WANAFUNZI WA MSINGI NA SEKONDARI

Mtendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya MTAKUWA, Kijiji cha Mtondo Kata ya Nambilanje, Abdala Mohamed akiwaelezea wanakijiji Mpango wa Serikali wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika mkutano wa selikari ya kijiji kuzungumzia masuala ya kijinsa na athari za mila potofu uliohudhuriwa na TAMWA ikiwa ni muendelezo wa ziara ya wiki  zima inayofanywa na TAMWA vijiji vya Wilaya ya RUWANGWA.

WAKAZI wa Kijiji cha Kitandi kilichopo Wilaya ya Ruangwa wamemuomba Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa kuweka katazo kali kwa manesi wa Ruangwa nzima kuacha kuwapa dawa za uzazi wa mpango watoto wa shule za msingi na sekondari.

Hayo yamesemwa Aprili 04, 2019 katika mdahalo wa kijiji ulioendeshwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) katika uwanja wa shule ya msingi kitandi unaohusu mila na desturi zinazopelekea madhara katika jamii. Hayo yametokana na kuwepo na malalamiko ya watoto wenye umri mdogo kuanza vitendo vya uasherati katika umri mdogo katika maeneo ya Ruangwa.

Mkazi wa kijiji cha kitandi Rashidi mang'omba amesema tatizo hili linaanzia nyumbani kwa kina mama kwani wao ndiyo wanawapeleka hospitali kuwekewa vipandikizi hii inawapa uhuru wa kufanya uesharati kwa uhuru zaidi.

Ombi langu kwa Mkuu wa Wilaya ni kuweka sheria kali kwa mzazi atakaebainika anamuwekea vipandikizi mwanae na hata nesi atakaetoa huduma hiyo kwa mwanafunzi achukuliwe hatua. Naye khalidi Selikali ameiomba Serikali ya kijiji kuwachukulia hatu.

No comments:

Post a Comment