WAFANYAKAZI VODACOM TANZANIA WATEMEBELEA SEKONDARI ZA WASICHANA ARUSHA DAY NA SANGU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Tuesday, 12 March 2019

WAFANYAKAZI VODACOM TANZANIA WATEMEBELEA SEKONDARI ZA WASICHANA ARUSHA DAY NA SANGU

Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa shule ya sekondari Arusha Day, Joyce Gyunah katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, Wafanyakazi wa Vodacom wametembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao. 

Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen akizungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Arusha Day na kuwahimiza kusoma kwa bidii, katika hafla iliyofanyika jijini Arusha jana. Katika kuadhimisha wiki ya wanawake duniani, kampuni ya Vodacom imetembelea shule hiyo ya wasichana na kuwapatia vifaa kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

Meneja  Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini, Magreth Lawrence (kushoto) akimkabidhi daftari, Jackline Chaula, mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Sangu jijini Mbeya. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wa kampuni hiyo wametembelea, kuongea na kutoa zawadi na vifaa mbalimbali kwa wasichana ili kuwasaidia mahitaji yao ya shule  ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao. 

Mkuu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen akizungumza na wanafunzi juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike. WAFANYAKAZI wa Vodacom Tanzania walitembelea shule ya Sangu, Mbeya na shule ya Arusha Day, katika kuadhimisha siku ya wananwake duniani na kutoa msaada wa vifaa vya mashuleni.

Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini, Magreth Lawrence, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Sangu juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wametembelea shule hiyo na kuwapatia vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao ya shule ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watoto wa kike wanafanya vizuri katika masomo na wanatimiza ndoto na malengo yao.

No comments:

Post a Comment