Mtangazaji maarufu, Ephraim Kibonde |
IMEPITA siku tisa tangu kituo cha Utangazaji cha Clouds
Media kupata pigo kwa kuondokewa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, wamepata pigo jingine baada ya
kuondokewa na mtangazaji wake maarufu, Ephraim Kibonde aliyekuwa akiendesha
kipindi cha Jahazi. Kifo cha mtangazaji huyo kimetokea Machi 7, 2019.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Kibonde amefariki akiwa
Mwanza na alianza kusumbuliwa na presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Ruge
na kulazimika kukimbizwa hospitali kabla ya kuhamishiwa jijini Mwanza alipo
kubwa na mauti hayo. Mwana ametoa na ametwaa jina lake lihimidiwe. Apumzike kwa
amani Kibonde. Amina
No comments:
Post a Comment