MISA TAN YAENDESHA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA KILIMANJAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 14 March 2019

MISA TAN YAENDESHA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA KILIMANJAR

  Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa Mahakama,mafunzo yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Misa tan katika Hotel Ya Leopard mjini Moshi.

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama mbalimbali katika mkoa wa Kilimanjaro wanaoshiriki mafunzo hayo.

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa Tan),Salome Kitomary akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumishi wa mahakama za mkoa wa Kilimanjaro.

Baadhi ya Watumishi wa mahakama wakishiriki mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Leopard mjini Moshi.

  Mkurugenzi wa Misa Tan, Gasirugwa Sengiyumva, akiwaleza washiriki wa mafunzo hayo shughuli mbalimbali ambazoo taasisi ya Misa Tan imekuwa ikifanya.

Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ,Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Patricia Fikirini pamoja na wakufunzi wakati wa ufunguzi rasimi wa mafunzo hayo.


Na Dixon Busagaga, Moshi

KAIMU Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini,amesema kuwa mafunzo ya huduma kwa wateja na upatikanaji wa taarifa kwa watumishi wa Mahakama ni muhimu kwa kuwa yatapunguza malalamiko kwa watumiaji wa mahakama.

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa mahakama za mkoa wa Kilimanjaro, Jaji Fikirini alisema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa limekuwa ni hitaji la muda mrefu.

Mafunzo hayo yameendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Misa tan, kwa kushirikiana na Taasisi ya Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung, yanahusu huduma kwa wateja, upatikanaji wa taarifa na maadili kwa utumishi wa umma.

“Mafunzo haya ni msingi wa mabadiliko kwa kilio kwa wateja kutoridhishwa na huduma za mahakama.Natarajia yatazingatiwa na kusaidia kuleta mabadiliko katika kuwahudumia wateja.”alisema Jaji Fikirini.

Aidha, aliwataka watumishi hao kuunda kukosi kazi cha ufuatiliaji wa utekelezaji wa mafunzo hayo ya jinsi wanavyowahudumia wateja wanaofika mahakamani, ili kupunguza malalamiko ambayo yanatoa taswira isiyo sahihi kwa mahakama.

Awali akimkaribisha Jaji Mfawidhi Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini, kufungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa Tan),Salome Kitomary alisema Misa Tan imepanga kutoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi hao wa mahakama.

Alisema mafunzo yatakayotolewa ni pamoja na huduma kwa wateja, upatikanaji wa taarifa na maadili kwa watumishi wa mahakama kwa Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mahakimu wa Mahakama za Wilaya, Mwanzo pamoja na watumishi wa mahakama na watunza kumbukubu 36 wa mkoa wa Kilimanjaro.

Kitomary alisema washiriki hao watafundishwa nini maana ya uhuru wa kujieleza (mambo muhimu na misingi yake), huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa umma.

Kadhalika, washiriki watajifunza mifano ya utekelezaji wa uhuru wa kujieleza, Tanzania, Afrika na Duniani, Matakwa ya kisheria ya uhuru wa upatikanaji wa taarifa, muundo wa vyombo/ taasisi za umma na upatikanaji wa taarifa.

Aidha, washiriki hao pia watajifunza jinsi ya kutoa taarifa na kuomba taarifa, ujuzi wa misingi na sifa za kushughulikia malalamiko ndani yake ikiwa ni muundo wa kushughulikia malalamiko,manufaa ya kushughulikia malalamiko kwa wakati, kukabiliana na tabia za ndani na jinsi ya kwuahudumia wateja wenye hulka tofauti na kukabiliana na malalamiko kiufundi katika kukabiliana na hasira na majibu yenye mhemko.

Mada nyingine zinazotarajiwa kuwasilishwa ni pamoja na kukabiliana na kazi zenye malalamiko ambayo ndani yake ina kukubaliana na hatua inayofaa kwa wateja, kuwa wazi juu ya mamlaka/nguvu ulizonazo, kuongezeka kwa malalamiko na mchakato wa usimamizi wa malalamiko, kutoka maoni na kuheshimu ahadi.

Kwa siku ya tatu washiriki watafundishwa au kukumbushwa juu ya kanuni za maadili na maadili kwa watumishi wa umma, utaratibu wa mahakama katika kushughulikia malalamiko.

Mkurugenzi wa Misa Tan, Gasirugwa Sengiyumva, alisema  chanzo cha mafunzo haya ni mwaka 2004 baada ya Mahakama kupata kufuli kwa kutofunguka kutoa taarifa kwa wananchi, utafiti huo ulifanywa na Misa Tan, ukiangalia taasisi za umma ambazo zimefungaka zaidi na ambazo hazikufunguka kutoa taarifa kwa wananchi wa kawaida kabisa.

No comments:

Post a Comment