KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MIUNDOMBINU NA KAMATI YA PAC ZAKAGUA MIRADI YA UJENZI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 13 March 2019

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MIUNDOMBINU NA KAMATI YA PAC ZAKAGUA MIRADI YA UJENZI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi Selemani Kakoso, akisisitiza jambo kwa  Naibu Mawaziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa na Mhe. Atashasta Nditiye, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Atashasta Nditiye, akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi Selemani Kakoso, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. 

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Bi. Bertha Bankwa, akielezea mkakati wa uboreshaji wa kiwanja hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokikagua.

Mhandisi Kedrick Chawe kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), akionesha ramani ya Kiwanja cha Ndege cha Msalato kitakavyokuwa mara baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi wake kukamilika kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua eneo ambalo kiwanja hicho kitajengwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka, akikagua ubora wa lami katika eneo la Nkulabi, barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260), wakati kamati hiyo ilipokagua barabara hiyo leo.

No comments:

Post a Comment