Hafla hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa vituo vya afya na
wadau mbalimbali kutoka ofisi za serikali. Programu hii ya “Fistula inatibika”
ilianza mwaka 2012 na imelenga kuwasaidia wanawake wanaoishi na hali ya fistula
kupata matibabu ya kiafya na kisaikolojia
kwa sababu wengi wao hutengwa na jamii zinazowazunguka kutokana na
ugonjwa huo, pamoja na kuwawezesha kurejea katika hali zao za kawaida na
kujumuika kwenye jamii zao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Vodacom
Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia alisema, “Mabalozi hawa wanaungana na
mabalozi wengine zaidi ya 3000 wa fistula waliopo sehemu mbalimbali nchini,
wenye uwezo wa kutambua na kuwawezesha waathirika wa Fistula kufika hospitali
ya CCBRT au vituo vingine vya afya vinavyotoa matibabu hayo kama; Bugando
(Mwanza), KCMC (Kilimanjaro), Nkinga (Tabora), Peramiho Mission Hospital
(Ruvuma), Kabanga Mission Hospital (Kigoma), Songea Regional Hospital (Ruvuma)
na Selian (Arusha) kwa kutumia mfumo wa M-Pesa.
Nawasihi mabalozi hawa kutoa mafunzo kwa jamii zao kuhusu
fistula kwa kuandaa semina ambazo zitaambatana na majadiliano ya changamoto
mbali mbali zinazotokana na fistula”.
Shirika la Afya duniani (WHO) linakadiria kwamba wanawake
3000 hupata tatizo la fistula kila mwaka nchini Tanzania. Hivyo mpango huu
ulianzishwa na Vodacom Tanzania Foundation kama sehemu ya kuisaidia serikali
kuboresha huduma za afya nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
“Fistula ni hali inayozuilika na kutibika hivyo inabidi
tuidhibiti kabisa. Katika karne hii hakuna mwanamke anayestahili kutengwa au
kunyanyapaliwa na jamii yake kwa sababu ya fistula. Ninapongeza juhudi za
taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation katika kukabiliana na matatizo ya kiafya
yatokanayo na uzazi nchini. Tunahitaji kukabiliana na mzigo huu wa akina mama
wenye matatizo haya katika jamii zetu,” alisema Afisa Mtendaji mkuu wa
hospitali ya CCBRT bi Brenda Msangi.
Wanawake wenye fistula wana changamoto kubwa ya kutengwa
katika jamii zao na wengi wao hawatambui kama hali hii inatibika kutokana na
ukosefu wa elimu na taarifa. Utumiaji wa mabalozi wa Fistula ni hatua muhimu
zaidi maana wao hutumika katika kuwatambua na kuwapa rufaa wanawake wanoishi na
hali ya Fistula.
“Mwaka wa kwanza baada ya kuanza kutumia M-pesa kutoka
Vodacom katika mfumo wetu wa rufaa tulishuhudia ongezeko la asilima 65 ya wanawake
waliotibiwa ugonjwa wa fistula, kufikia mwaka 2016, asilimia 87 ya wagonjwa wa
fistula walipata rufaa kupitia mfumo wa M-Pesa ambao tunashirikiana na Vodacom
Tanzania Foundation, wakafanikiwa kufika CCBRT ambapo tulifanya upasuaji wa
wagonjwa 1,012”, aliongeza Bi Msangi.
No comments:
Post a Comment