MWILI WA RUGE MUTAHABA KUWASILI TANZANIA MACHI 1,2019 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 28 February 2019

MWILI WA RUGE MUTAHABA KUWASILI TANZANIA MACHI 1,2019

Ruge Mutahaba
MWILI wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba unatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Ijumaa ya Machi 1,2019. Taarifa kutoka kwa msemaji wa familia, Annik Kashasha zinasema taratibu za kuurejesha mwili kutoka nchini Afrika Kusini zimeanza na mazishi yatafanyika Bukoba, mkoani Kagera wiki ijayo.

“Mwili wa marehemu utarejeshwa hapa nchini siku ya Ijumaa (Machi 1) na siku ya Jumapili (Machi 3) utasafirishwa kwenda Bukoba kwaajili ya mazishi. Kashasha amesema shughuli za kumuaga Ruge ambaye ni mwanzilishi wa semina za fursa zitafanyika siku ya Jumamosi.

Historia fupi:
Ruge alizaliwa Brooklyn New York Marekani mwaka 1970, Primary School amesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha akahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo alipomaliza darasa la saba.

Kisha akasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo akarudi Marekani ambako alienda kusoma San Jose University California ambako alichukua BA in Marketing na BA in Finance, kozi zote alisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo akarudi tena Tanzania.

Kuanzishwa kwa Clouds FM:
Wakati yupo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, yeye Ruge akawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo waka-build good friendship. Sasa, aloporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yake, Joseph Kusaga akamshawishi sana abaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo alipojikuta yupo Clouds Entertainment.

Taarifa za awali zinabainisha kuwa Mutahaba ameacha watoto wawili (Juju) na (Shubi) ambao aliwapata na Zamaradi Mketema. Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo Mutahaba alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo, kwa maana hiyo alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu hadi mauti yalipomfika tarehe 26 Februari 2019.

No comments:

Post a Comment