Bw. Everest Michael, Mwenyekiti Mpya. |
Bi. Jocylne Devosta, Mweka Hazina wa umoja huo. |
Bw. Godfrey Mwamsoyo, Katibu Mkuu wa umoja huo. |
KWA mujibu wa taarifa toka Jumuiya ijulikanayo kamaTanzanians Dallas, ambayo ni jamii ya watanzania wanaoishi katika
jiji la Dallas, Texas na vitongoji vyake, limefanya mabadiliko siku ya Jumamosi
tarehe 12, 2019 kwa kuwachagua viongozi mpito watatu. Uchaguzi huo ulihudhuliwa
na wakazi wengi wa sehemu hizo zilizolizunguuka jiji la Dallas na kufanya
maamuzi ya uongozi wa dharura kutokana na kujiudhuru kwa uongozi uliyopita.
Watanzania
katika jiji hilo la Dallas na vitongoji vyake wanaamini kwamba, mshikamano wao
ambao ndio kilikuwa ni chanzo kikubwa cha wao kuwa kitu kimoja wakati wa misiba
na dharura za aina yote kimaishi wanavyoishi huko ughabuni. Kufuatana na katiba
ya jumuiya hiyo hakuwa nabudi kuitisha kikao na kuwa na maamuzi ya kuteuwa
wagombea mpito mpaka hapo mwezi Julai katika uchaguzi mkuu chini ya utaratibu mpya.
Uongozi
uliotumikia jumuiya hiyo kwa muda sasa na hatimae kujiudhuru kwa hiyari, ni
mwenyekiti Bw. Benedict Kazora, Bi Maria Musomi, Makamo mwenyetkiti na Bi
Viola mbise, Katibu. Maamuzi hayo ya
ghafla yaliwakilishwa kwenye kamati ya ushauri na kutangazwa rasmi katika
tofuti za mitandao ya kijamii mara moja. Harakati zipo mbioni kuwasiliana na
uongozi uliopita kukabidhiana nyaraka na uongozi mpya mpito haraka
iwezekanovyo.
Jumuiya
hiyo, imewachagua viongozi wake mpito wapya kupitia utaratibu wa kuwapigia kura
wale wote walioteuliwa na wanajumuiya baada ya mkutano huo mahususi kuziba hizo nafasi hizo. Yafuatayo ni majina
ya wachaguliwa wapya, Mwenyekiti ni Bw.
Everest M. Michael, Katibu Bw. Godfrey Mwamsoyo na mweka hazina ni Bi Jocyline
Vadesto. Wateuliwa wote hao ni wakazi wa Dallas na vitongoji vyake. Jumuiya
mzima ya Watanzania Dallas inatoa pongezi na shukrani nyingi kwa wale wote
walio pata wasaa na kujitokeza kufanya zoezi hili muhimu.
Pia
vilevile, sambamba na mkutano huo lilichaguliwa baraza la ushuri la watu wa
jumuiya hiyo chini ya mapendekezo ya
wanajumuiya wake, na sio tena kama jinsi baraza lile la zamani kuteuliwa na
mwenyekiti. Hii ni kuhamasisha dhamira
na malengo ya jamii kupewa
kipaumbele katika maswala ya jamii hiyo. Misiba na matatizo yasiyo tabirika,
ndivyo vigezo vikuu vilivyo waleta wanajumuiya hao pamoja na kusaidiana kutatua yanayojiri wakati kama huo mgumu
kwao.
Hivyo
basi, baraza la ushauri lina takribani watu kumi na moja ambao watakuwa na
mawasiliano ya mara kwa mara na uongozi wa juu na kujaribu kuwa na ufumbuzi wa
matitizo au misiba inapotokea katika uzio wa mipaka ya vitongoji vyao. Hivyo, walioteuliwa
na jamii hiyo katika baraza au kamati hiyo hadi hapo mwezi Julai uchaguzi mkuu ni:
1.
Bw.
AloyceChissanga; 2. Bw. Peter Kapanga; 3. Bi Anna Ngoti; 4.Bw. Felix Maganjila;
5. Bw. Kibwana Rumadha; 6. Bi Arafa Manganji; 7. Bw. Ibrahim Kulindwa; 8. Bi Rosemary
Kessy; 9. Bw. Erick Joshua; 10. Bi Sofia Lesso; na 11. Bw. Godlisten Lyimo.
Hao ndio wanaoiwakilisha baraza au
kamati ya ushuri mpito iliyopo madarakani tokea uchaguzi wake wa tarehe 12January mwaka 2019.
Juhudi zinaendelea kuhakikisha kwamba
kwa mujibu wa katiba, yote yanayojiri katika makabidhiano ya kifedha na vitega
uchumi ya Jumuiya vinatendwa chini ya utaratibu sahihi na wenye nidhamu. Hii
utawapo urahisi fasaha wale viongozi wapya kufuatialia harakati zote zinazo husiana
na jumuiya na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia vivutio vyake asilia vya
kitalii na maliasili.
Kwa mujibu wa taarifa toka kwa
mwenyekiti mpya wa mpito, ndugu Everest, inaeleza kwamba, kazi kubwa iliyopo ni kuwa
hamasisha wanajumuiya wote wa asili ya Tanzania kushiriki katika ufumbuzi wa
maswala yanayotukabiri na kuwa bora, imara zaidi ya jumuiya zinginezo toka
Afrika. Tanzania, hususani sekta ya utalii, madini na nyanja nyinginezo tofauti, tutazidi kuwa mstari wa mbele
kuhakikisha nchi yetu inazidi kutambulika hapa na kuwavutia jamaa na marafiki
wetu wa Marekani waje tembelea mbuga
zetu za wanyama, mlima wa Kilimanjaro na
mengineyo zaidi toka Tanzania.
Mwisho kabisa, Jumuiya hiyo ya
watanzania wanaoishi Dallas na vitongoji vyake vya karibu pia
wakazi wake ambao kwa namna moja au nyingine waliowahi kuishi huko
wanawatakia uongozi huu mafanikio mema yenye mshikamano wa dhati na uzalando halisia kama Tanzania Diaspora.
No comments:
Post a Comment