Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel leo jijini Dar es Salaam. |
. Malengo ni kuwafikia wateja wa Halopesa 1.5 million 2019
JANUARI 2, 2018 ulikuwa
mwaka mzuri kwa Kampuni ya Halotel Tanzania ikiwa moja ya Kampuni ya
Mawasiliano iliyosajiliwa nchini ikifanikiwa kuongeza idadi ya wateja na
mawasiliano katika maeno mbalimbali nchini.
Takwimu zilizopo zinaonyesha watumiaji wa mtandao wa Halotel hadi
Septemba imeweza kufikia wateja Milioni 4 ikikua kutoka wateja 3.7 Milioni
Septemba Mwaka 2017 .Halkadhalika idadi ya watumiaji wa Halopesa ikionekana
kuongezeka kwa kasi kutoka watumiaji 358,217 Septemba Mwaka 2017 hadi
watumiaji 800,000 Septemba Mwaka 2018.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
Nguyen Van Son, kuongezeka kwa mafanikio hayo ya Kampuni hiyo hususani
katika huduma za watumiaji wa Halopesa kumetokana na mpango wa utoaji huduma
kwa wateja uliozinduliwa na Kampuni mapema Mwaka 2018.
“Kwa kifupi kamopuni imeweza kukua katika utoaji wa huduma zake
mbalimbali kwa kipindi chote cha mwaka uliopita, katika kipindi hicho
Halotel imezindua huduma mbalimbali ikiwemo huduma shirikishi inayomwezesha
mteja kutuma au kupokea Fedha kutoka Halopesa kwenda katika akaunti yake au
mtandao mwingine wowote wa simu; pia tulizindua huduma ya utoaji
mkopo ijulikanayo kama ‘HaloYako’.
“Aidha katika kipindi hicho pia
tulikuja na mpango wa ulipaji malipo mbalimbali Serikalini kumwezesha mteja
kuondokana na usumbufu mbali na hiyo pia tumeweza kumrahisishia mteja kuweza
kutuma fedha katika benki zaidi ya 20 zilizopo nchini” alisema Son.
HaloPesa ilikuwa na mawakala hai
wapatoa 10,367 Mwaka 2017 lakini hadi tunapozungumza hivi sasa idadi hiyo
imeongezeka na kufikia Mawakala 155,000 nchini kote.
Aidha alisema mapato yaliyotokana na
thamani ya manunuzi ya HaloPesa pia yaliongezeka hadi kuifikia 183%,
"Tuliona kiwango cha 356% katika thamani ya manunuzi ya HaloPesa na
ongezeko kwa 167% alisema.
Mafaniko hayo yalitokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Halotel kwa
kuweka miundombinu katika maeneo mbambali nchini katika kipindi cha Mwaka 2018.
Alisema hatua hiyo ilichangiwa na ushirikiano wa kampuni hiyo na
Serikali hasa katika utekelezaji wa awamu ya pili ya uboreshaji wa
mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ulioiwezesha Halotel
kufiksha mawasiliano katika Vijiji 240 katika kipindi cha Mwaka jana.
Kampuni pia imeweza kuunganisha mawasiliano kupitia mkongo zenye urefu
wa Kilomita 2000 katika maeneo yenye miundombinu yake kwa ajili ya kuwezesha
upatikanaji wa data kwa maeneo mapya; kupitia hilo Halotel imeendelea kuwa
chaguo la kwanza kwa wateja pale linapokuja suala la huduma za Intaneti.
“Hii ndio sababu tumeweza kuongeza dakika zaidi za kupiga kwenda katika
mitandao yote hasa kupitia kifurushi cha kila kikimpta mteja unafuu wa hadi
asilimia 32% lengo ni kumpa mteja kitu anachostahili kupitia ofa hiii maalumu
ni hii ilitokana na mahitaji hasa kwa wateja wa Dar es Salaam na Manyara”
alisema Son.
Akizingumzia malengo ya mwaka 2019, “Tunaamini kuwa Mwaka huu utakuwa ni
wenye mafanikio makubwa kwa Halotel na Halopesa kwa ujumla tukilenga
kuwafikia wateja zaidi 1.5 Milioni ifikapo mwisho wa mwaka 2019. Aliongeza Son.
Alisema chini ya utekelezaji wa mpango
wa awamu ya tatu ya UCSAF iliousaini Desemba Mwaka 2018, Halotel inatarajia
kufikisha mawasiliano na kuviunganisha vijiji zaidi 328 nchi nzima.
Kupitia hatua hiyo anaamini
kampuni itazidi kuweka maboresho katika huduma za kifedha kupitia mtandao
mara mbili zaidi. Alisema pia Halotel pia itazindua
ufumbuzi zaidi wa malipo, na zaidi ikijipanga kuendelea h kuwa kiongozi katika
ufumbuzi wa ICT nchini.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel leo jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment