MSD YARAHISISHA UPATIKANAJI TAARIFA ZA DAWA, VIFAA TIBA NA VITENDANISHI VYA MAABARA KIDIGITALI. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 9 November 2018

MSD YARAHISISHA UPATIKANAJI TAARIFA ZA DAWA, VIFAA TIBA NA VITENDANISHI VYA MAABARA KIDIGITALI.



BOHARI ya Dawa MSD imerahisisha mfumo wa upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wateja wake,ambazo ni pamoja na taarifa za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD.

Taarifa hizo zinapatikana kwenye mfumo maalum wa kieletroniki/kidigitali  unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali wakati wakuagiza dawa, ambapo ili walazimu kusafiri ofisi za Kanda ya MSD inayowahudumia/ au kupiga simu ili kupata taarifa hizo na nyinginezo.

Akizungumzia mfumo huo jana, Kaimu Mkurugenziwa Tehama wa MSD Bw. Pascal Pastory alisema kupitia mfumo huu, MSD imedhamiria kuongeza ufanisi katika kuhudumia vituo vya kutolea hudumaza afya nchini ili kuhakikisha adhma ya serikali ya awamu ya tano ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi inatimizwa kwa vitendo.

“Mfumo huu unalenga kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wataarifa muhimu zihusuzo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vinavyotolewa na MSD kwa vituo vya kutolea huduma za afyanchini, kwa kuviwezesha vituo hivi kupata taarifa muhimu zihusuzo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa wakati popote walipo nchini hata kupitia simu zao za mkononi” alisema Bw. Pastory.

Aliongeza kuwa mfumo huu, utawawezesha wateja wa MSD kupata taarifa za upatikanaji wa dawa ghalani (stock status) iliiwerahisi kwao kuagiza mahitajiyao MSD kulingana na matakwayaokwawakatihusikahata pale wanapokuwa na mahitajiya dharura.

“Mfumo huu utawasaidia wateja wa MSD kupata taratibu za maombiya dawa(order processing status) kutoka Makao Makuu, Ofisi za Kanda, Vituo vya mauzo vya MSD,jambo ambalo litawaondolea usumbufu wa kusafiri kupata maelekezo, kwa kuwa mfumo huu unataarifa zote muhimu juu ya namna ya kupata mahitaji yao kutoka MSD” alisisitiza Bw. Pastory.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa Tehama aliongezakuwawatejawa MSD wataweza kufahamu bei ya dawa (item price) mbalimbali zinazopatikana kwa wakati husika katika maghala ya MSD, kwani taarifa hizi ni muhimu kwao wakati wakupanga bajeti zao za manunuzi, na kufanya nakisi ya kiasi gani kitumike kununulia dawa husika.

Sambamba na hayo, alidokeza kuwa mfumo huo utawawezesha wateja wa MSD kupata taarifa za miamala yao (customer statement) ili wafahamu kiasi cha pesa kilichopo kwenye akaunti za o MSD na kiasicha fedha kilichotumika kununulia dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kwa wakatigani.

Kwa kufanyahivyo, mfumo huu utakuwa umeondoa sintofahamu zilizokuwa zikijitokeza kipindi cha nyuma,kwa kuwa mfumo huu ni wazi na rahisi kutumia.

Kwa mujibu wa Patory mbali na faida hizo, mfumo huu unawawezesha wateja wa MSD kutoa mrejesho wa huduma wanazopata kupitia fomu maalumu zilizoko ndani ya mfumo huu. 
Taarifa hizo zitakusanywa na watalaamu ilizisaidie kuboresha huduma kwa siku za usoni, kwani maoni na mapendekezo ya wateja yatakuwa yakipatiwa utatuzi kadri yatakavyo kuwa yakitolewa.

Naye mfamasia kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoawa Tabora- Kitete, Samson Mrema alisema walijiunga na mfumo huu miezi ya hivi karibuni na wamenufaika sana, kwani hawahitaji kusafiri tena kufuata taarifa kwa kuwa kila Kitu kinapatikana kupitia mtandaowa “MSD Customer Portal” 

Aidha aliwataka wateja wengine wa Mkoa wa Tabora wajiunge na mfumo huo kwa ni nirahisi kuutumia hata kupitia simu janja (smartphone) na unaokoa muda kwa kuwa kila taarifa muhimu inayohusu upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, na vitendanishi vya maabara kwenye maghala ya MSD imerahishishwa.

No comments:

Post a Comment