BIASHARA NDOGO NA ZA KATI NI MUHIMU KATIKA KUKUZA KIPATO NA UCHUMI NCHINI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 9 November 2018

BIASHARA NDOGO NA ZA KATI NI MUHIMU KATIKA KUKUZA KIPATO NA UCHUMI NCHINI

ogo na za Kati ni muhimu katika kukuza kipato na uchumi nchini









Si kwa hapa Tanzania tu hata sehemu nyinginezo duniani wafanyabiashara wameshaanza
maandalizi ya ofa za mauzo ya mwisho wa mwaka.

Tayari maduka na wafanyabiashara wameshaanza kuweka matangazo
ya ofa za bidhaa walizonazo. Kipindi hiki huwa na pilikapilika nyingi kwa
sababu ni kipindi ambacho wafanyabiashara hufanya mauzo
makubwa na kupata faida pengine kuliko msimu wowote ndani
ya mwaka wote.

Kuelekea msimu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya huwa ni
kipindi ambacho watu hufanya manunuzi ya bidhaa tofauti kwa
ajili ya familia, ndugu na jamaa zao. Bidhaa nyingi huwa katika
ofa na mapunguzo hivyo kutoa fursa kwa wateja kufanya manunuzi
kwa unafuu.

Watu wengi husubiria msimu huu kufanya manunuzi kwa sababu
wanakuwa na uwezo wa kupata bidhaa nyingi na tofauti kwa
gharama nafuu. Kwa hiyo, ni msimu ambao huwa unasubiriwa
kwa hamu na wateja sehemu mbalimbali duniani.

Kwa hapa nyumbani Tanzania, Jumia kupitia kampeni yake ya
Black Friday ambayo itaanza Novemba 16 mpaka Desemba 7,
itawawezesha watanzania kufanya manunuzi muda na mahali
popote walipo huku wakisubiria kuletewa bidhaa zao mpaka walipo.
Yaani itakuwa ni Black Friday kila Ijumaa na kuwawezesha
wateja kununua chochote walichokifikiria akilini mwao kabla
ya msimu wa sikukuu!
Jumia, ambalo ni duka la bidhaa mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara
tofauti mtandaoni huwa na kawaida ya kufanya kampeni hii kubwa ya mauzo
katika mwaka. Kwa kawaida Black Friday huwa inafanyika Novemba 23 ya
kila mwaka, lakini kwa mwaka huu itakuwa ni kwa Ijumaa nne mfululizo.
Wateja wa Jumia watakuwa na fursa ya kunufaika kwa kununua bidhaa
mbalimbali kwa bei nafuu, kupewa ofa, mapunguzo mpaka 70%, na zawadi lukuki!

Akizungumzia namna Black Friday itakavyowafaidisha wafanyabiashara
na wateja, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James amesema kuwa,
“Hiki ni kipindi ambacho wafanyabiashara mbalimbali wanaweza kukitumia kujitangaza,
kujiongezea masoko, wateja na faida kubwa katika biashara zao.

Jumia ni mtandao pekee ambao unatembelewa na wateja wengi kutoka sehemu tofauti.
Hakuna gharama zozote kwa ajili ya mfanyabishara kujiunga nasi, kujitangaza au usafiri wa
bidhaa kwenda kwa wateja. Hivyo basi, badala ya wafanyabiashara kuingia gharama za
kufanya yote hayo au kutegemea wateja kutembelea madukani mwao moja kwa moja ni
vema wakaitumia fursa hii kukuza biashara zao.”

“Wateja nao wana fursa ya kufanya manunuzi muda na mahali popote ili mradi wawe
wameunganishwa na huduma ya intaneti.

Wanaweza kufanya manunuzi kupitia tovuti ya Jumia kwa kutumia kompyuta,
tabiti au kwa App ya simu za mkononi.

Ofa na mapunguzo ni nyingi kwa bidhaa za aina mbalimbali kama vile kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani, maofisini, shuleni, michezo na burudani, vifaa vya umeme,
mavazi na mitindo mbalimbali pamoja na kupelekewa mpaka walipo bure kabisa!”     

Black Friday ni msimu ambao wafanyabiashara na wateja wa nchini wa Tanzania
wanapaswa kuutumia ipasavyo kwa ajili ya mauzo na manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Lakini pia unatoa fursa kwa kukua kwa sekta ya biashara kwa njia ya mtandaoni ambayo
imeshika hatamu duniani kote.

Mfumo huu unarahisisha manunuzi, kutanua masoko, kuongeza wateja
na faida ambayo ni muhimu katika kukuza kipato na uchumi.  

No comments:

Post a Comment