MIPANGO MIJI INAPASWA KUENDANA NA SERA YA UJENZI WA VIWANDA NCHINI–PROF. MAKENE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 30 November 2018

MIPANGO MIJI INAPASWA KUENDANA NA SERA YA UJENZI WA VIWANDA NCHINI–PROF. MAKENE

index
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akizungumza na washiriki (hawapo pichani) katika mkutano wa kuwasilisha Mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

3
Mkuu wa Mkakati wa Utafiti na Machapisho kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Prof Fortunata Makene akitoa semina kwa washiriki (hawapo pichani) katika mkutano wa kuwasilisha mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

4
Mgeni rasmi Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kuwasilisha mwongozo mfupi wa maendeleo ya mijini nchini uliofanyika katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) akisisitiza jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji makazi holela toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.Betha Mlonda kulia ni Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu katika mkutano wa kuwasilisha Mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

G-min
Kamishna Msaidizi wa Sera katika Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael Nyagoga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa kuwasilisha Mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

6
Akizungumzia uzoefu wake kutoka katika Kituo cha Afrika cha Maendeleo ya Majiji cha Afrika Kusini,Bw. Anton Cartwright katika mkutano wa kuwasilisha Mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika Hotel ya Morena jijini Dodoma. 

A
Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji makazi holela toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.Betha Mlonda akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano wa kuwasilisha Mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

C

Mkuu wa Mkakati wa Utafiti na Machapisho kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Prof Fortunata Makene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa kuwasilisha mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

 D-min
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk Nathalie Jean-Baptite akitoa semina kwa washiriki wa mkutano wa kuwasilisha mwongozo mfupi wa maendeleo ya miji nchini uliofanyika katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.
..............................
Na.Alex Sonna, Dodoma

IMEELEZWA kuwa mipango ya Miji na ujenzi wa Miji nchini unatakiwa kwenda sambamba na mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya kuwa nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Kuwasilisha Mwongozo Mfupi wa Maendeleo ya Miji nchini, Mkuu wa Mkakati wa Utafiti na Machapisho kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Prof Fortunata Makene amesema kuwa mikakati ya mipango miji inatakiwa kuzingatia malengo hayo ya kitaifa.
Alisema ESRT imewasilisha Mwongozo ambao umeletwa kwa wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za umma na binafsi kwa lengo la kuuchambua na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuweka mipango madhubuti inayoendana na kasi ya ukuaji miji hiyo nchini.
“Mwongozo huo mfupi ambao unaenda sambamba na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe, unaonesha wazi kuna kila sababu ya kuainisha upangaji miji na kasi ya ukuaji wa miji hiyo”alisema.
Alisema ESRF inaonesha wazi katika utafiti huo serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ndiye mwenyekiti wa kuwezesha taasisi nyingine kutekeleza mipango miji hiyo nchini, ipo kwa ajili ya kusikiliza wadau nini kifanyike mipango miji iendane kasi ya ukuaji miji.
“Ukiacha wadau wa ndani, ESRF iliwaleta pamoja wadau kutoka Uingereza na Afrika Kusini (S.A) lengo ni kupata uzoefu wa namna ya kuweka malengo ya kuipanga miji ili kutopitwa na kasi ya ukuaji wa miji hiyo”alisema.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Sera katika Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Michael Nyagoga alisema serikali ndiyo mwenyekiti wa kusikiliza maoni ya wadau namna itakayotakiwa kuchangia kupitia sekta zake katika kutekeleza Mwongozo mfupi unaolenga kuepusha athari za miji kushindwa kupanga makazi kwa kuzindiwa na kasi ya ukuaji wake.
“Sisi kama serikali tunatakiwa kuwasikia wadau kuhusu mwongozo huo Mfupi ambao umeandaliwa ili kuona ni namna gani itachangia kwa kutoa fedha, utalaamu na msaada mwingine ili kufanikisha azma ya mipango ya ujenzi wa miji bora”alisema Nyagoga.
Aidha alisema serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais-Utumishi na nyingine wapo tayari kusaidia kadiri wadau watakavyo changia na wakashauri isaidie kufikia malengo.
Akizungumzia uzoefu wake kutoka katika Kituo cha Afrika cha Maendeleo ya Majiji cha Afrika Kusini, Anton Cartwright alisema Tanzania ina kila sababu ya kufanikisha mipango ya kujenga majiji yake kuendana na kasi ya watu kuhamia mijini kwa kutumia rasilimali zake.
“Inatakiwa kuweka kipaumbele kwamba ukuaji wa miji unatakiwa kuwa kitovu cha maendeleo ya nchi pamoja na kwamba itakuwa na raslimali nyingine,” alisema.
Vilevile alisema kuwa Tanzania imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi zikiwemo za kukua uchumi, gesi na mafuta na nyinginezo, hivyo maendeleo hayo yanatakiwa kuangalia ukuaji wa miji hiyo.
Akitoa utafiti wake kupitia filamu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk Nathalie Jean-Baptite alisema ukuaji wa mji wowote unatakiwa kwenda sambamba na maendeleo ya huduma, kwani wananchi wanataka kupata huduma bora wala hawaangalii zaidi fedha au malipo.

No comments:

Post a Comment