KATIBU MKUU KILIMO ATAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO GMO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 22 November 2018

KATIBU MKUU KILIMO ATAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO GMO

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

Na Mathias Canal, Dodoma

KATIBU Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 21 Novemba 2018 ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti na majaribio ya uhandisijeni (Genetic Modified Organism-GMO) yanayofanyika kwenye vituo vyake vya utafiti.

Aidha, Katibu Mkuu ameilekeza Taasisi hiyo ya TARI kuwa mabaki yote ya majaribio ya Uhandisijeni yateketezwe mara moja. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali.

Siku za hivi karibuni Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha Makutupora imekuwa inaalika watu mbalimbali kwenda kuona matokeo ya utafiti wakati serikali haijaruhusu matumizi ya uhandisijeni nchini.

No comments:

Post a Comment