RAIS MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YA MILIONI 20 KWA WAVUVI, MAMA JANETH ATOA MILIONI 5 ZA MAMA LISHE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Tuesday, 2 October 2018

RAIS MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YA MILIONI 20 KWA WAVUVI, MAMA JANETH ATOA MILIONI 5 ZA MAMA LISHE

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani (kulia) fedha za ujenzi wa ofisi za umoja huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza kiongozi wa Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga akishukuru baaada ya kupokea shilingi milioni 5 kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwaangalia Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga wakiweka sahihi katika hati za makabidhiano ya fedha taslimu kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli huku wakishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama na mshauri wa Rais Masuala ya sheria Bw. Dunstan Kiobya (kushoto) PICHA NA IKULU.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani wakielekea sehemu itapojengwa ofisi zao katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza kiongozi wa Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga akishukuru baaada ya kupokea shilingi milioni 5 kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani wakielekea sehemu itapojengwa ofisi zao katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Wajasiriamali wakishangilia kwa furaha utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na ya Mama Janeth Magufuli ya kutoa msaada wa shilingi milioni 5 kwa kia na mama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment