BILIONEA MO APATIKANA, POLISI WAAPA KUWANASA WALIOMTEKA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 21 October 2018

BILIONEA MO APATIKANA, POLISI WAAPA KUWANASA WALIOMTEKA...!

Mo Dewji

MO Dewji, bilionea Mtanzania aliyetekwa na watu wasiojulikana Alhamisi wiki iliyopita, amerejea nyumbani salama. Katika ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa kampuni yake, amesema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama."

Ujumbe huo umeandikwa kati ya saa tisa na robo alfajiri, na umeelekezwa kwamba umeandikwa kutoka Dar es Salaam. Gari alilotekewa Mo Dewji limesajiliwa Msumbiji.

Waziri wa Muungano na Mazingira Tanzania Januari Makamba naye ameandika kwenye Twitter kwamba: "Mohammed Dewji amerudi salama. Nimezungumza naye kwa simu dakika 20 zilizopita. Sauti yake inaonyesha yu mzima bukheri wa afya. Shukrani kwa wote kwa dua na sala. Naenda nyumbani kwake kumuona muda huu."

POLISI waapa kuwanasa waliomteka Mo Dewji Polisi nchini Tanzania wamesema watafanya kila wawezalo kuwatia nguvuni watu waliomteka na kumshikilia bilionea Mohammed Deji, Mo, kwa siku tisa.

Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amewaambia waandishi wa habari hii leo Oktoba 20 kuwa kuachiwa kwa Mo ni mwanzo wa kuwanasa wahalifu hao na kuahidi kuwapata wakiwa wazima au wamekufa.

"Mbio ukizianza sharti uzimalize. Huu ni mwanzo tu. Hao wahalifu wanaotaka kuchafua jina la nchi yetu lazima tuwatie nguvuni."

Sirro amesema upelelezi umeimarishwa kwa kushirikiana na mtandao wa polisi wa kimataifa Interpol.

"Nataka niwaambie (wahalifu) yawezekana wananisikiliza hivi sasa kuwa, popote watakapoenda tutawanasa. Wakienda Afrika Kusini tunao, Kenya tunao, Uganda tunao hata Msumbiji, popote pale tutawakamata maana tayari tunaushirikiano na wenzetu."

Sirro: Wahalifu walijaribu kuchoma moto gari
Mkuu wa jeshi la polisi Simon Sirro amesema wahalifu walijaribu kuchoma moto gari lilotumika kumtekea bilionea Mohammed Dewji.

Akiongea na waandishi wa habari asubuhi hii Sirro, amesema mara baada ya kumuachia, wahalifu hao walijaribu kuharibu ushahidi kwa kulichoma gari hilo lakini ilishindikana.

"Mkienda pale eneo la tukio mtaliona hilo gari, kuna madumu ya mafuta, walijaribu kuliwasha moto lakini ikashindikana.”

Sirro amesema wahehakiki gari hilo na kugundua gari hilo ndilo ambalo walikuwa wakilishuku kutumika katika mkasa wa kumteka bilione a huyo siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita.

Pia amesema walikuta bunduki na risasi katika gari hilo.

Hakuna aliyekamatwa mpaka sasa lakini uchunguzi bado unaendelea.


Gari lililotumika kumteka Mo Dewji lapatikana

Gari ambalo linaaminika kutumika katika kumteka bilionea Mohammed Dewji, Mo limepatikana kando ya viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ambapo bilionea huyo aliachiwa huru.

Jana, Mkuu wa polisi Tanzania IGP Simon Sirro alisema gari hilo, Toyota Surf, liliingia Tanzania likitokea nchi jirani mnamo Septemba mosi 2018.

Sirro hakusema gari hilo lilitokea nchi gani, lakini kutokanana na namba zake za usajili AGX 404 MC, BBC ilifanya uchunguzi na kugundua ni nambari za usajili za nchi ya Msumbiji iliyopo kusini mwa Tanzania.

Hata hivyo, gari hilo hii leo limeonekana likiwa na namba za usajili wa Tanzania T 314 AXX. Bado haijafahamika namba hizo za usajili wa Tanzania ni feki ama la.

Hakuna mtu aliyekamatwa, na bado haijulikani watu waliomtelekza Mo eneo hilo walitumia usafiri gani kutoroka.



Mo Dewji


Mo Dewji: Ninawashukuru Watanzania kwa kuniombea

Afisa mkuu wa polisi wa kanda ya Dar es salaam Lazaro Mombasa aliyetembelea nyumbani kwao Dewji kuthibitisha kurejea kwake nyumbani, watu waliomkamata walikuwa na lafudhi ya mojawapo ya lugha za mataifa ya Afrika Kusini. Aliongezea kwamba hatua hiyo imethibitisha wazi kwamba waliomteka sio watanzania.

''Nataka kuuthibitishia umma wa Tanzania kwamba nimefika nyumbani kwa akina Mo Dewji nimeongea naye niko na kikosi cha makachero hapa na ndugu yetu ni mzima kama IGP alivyozungumza na umma kwamba jeshi la polisi litaendelea na uchunguzi ili kuhakikisha kwamba tunampata muhusika akiwa mzima.

Mo Dewji ambaye alionekana mchovu alimshukuru mwenyezi mungu na serikali ya rais Pombe Magufuli pamoja na Watanzania kwa kumuombea.

''Namshkuru mwenyezi mungu , serikali ya magufuli na IGP , ahsanteni mimi ni mzima nawashukuru Watanzania wote kwa kuniombea.

Babake Mo alivimbia vyombo vya habari kwamba mwendo wa saa nane alifajiri walipokea simu ya Mo kwamba yuko salama na moja kwa moja wakaelekea katika eneo la Gymkhana ambako alikuwa amewachwa na watekaji wake.

'' Tumshukuru mwenyezi Mungu kwamba tumempata salama na anaendelea vizuri. Walikuwa wamemuacha pale na kuondoka. Lakini alikuwa hajafungwa na yuko sawasawa. Tunawashukuru Watanzania wote na rais''.

BBC

No comments:

Post a Comment