RAIS MAGUFULI AMPA KAMISHNA DIWANI ATHUMANI UKURUGENZI TAKUKURU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 6 September 2018

RAIS MAGUFULI AMPA KAMISHNA DIWANI ATHUMANI UKURUGENZI TAKUKURU

Kamishna Diwani Athumani.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani unaanza tarehe 06 Septemba, 2018.
Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani Athumani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
Kamishna Diwani Athumani anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Musoma, 06 Septemba, 2018

No comments:

Post a Comment