Kinachosababisha Ajali Mbaya Kwenye Barabara Zetu.. (1) - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 7 August 2018

Kinachosababisha Ajali Mbaya Kwenye Barabara Zetu.. (1)

Moja ya magari ya abiria katika ajali


Ndugu zangu,

TAIFA kwa mara nyingine tena limekumbwa na huzuni kubwa kwa matukio ya ajali. Ajali za hivi karibuni, mbali ya wengine, zimeua wanahabari wawili na kumjeruhi Waziri wa Serikali.

Nini hasa kinachangia ajali hizi?

Pamoja na kwamba yeyote yule anaweza kukumbwa na ajali ya bahati mbaya, lakini, ajali nyingi hutokana na uzembe wa madereva.

Sababu moja kubwa ya matukio ya ajali mbaya ni mwendo kasi. Kuendesha gari kwa kasi ni uzembe wa kwa dereva. Gari ikipata ajali kwenye mwendo kasi madhara huwa ni makubwa zaidi kuliko gari iliyopata ajali ikiwa kwenye spidi inayotakiwa katika eneo husika la barabara.

Bahati mbaya madereva wetu wengine hudhani ni sifa kuendesha gari kwa kasi. Hakuna kilicho kikubwa kwa dereva na abiria wake kama kufika salama.

Umefika wakati, tuweke utaratibu wa pale dereva anapokamatwa kuendesha kwa mwendo kasi zaidi ya mara mbili ndani ya mwezi mmoja, basi, dereva huyo anyang'anywe leseni yake na apewe adhabu ya kifungo cha nje japo kwa mwezi mmoja. Kisha arudie upya mafunzo ya udereva. Taratibu kama hiyo itekelezwe bila kujali kama huyo ni dereva wa Waziri au Mkurugenzi wa Shirika la Umma.

Ni bahati mbaya, baadhi ya madereva wa magari ya Serikali, tena wakiwa wamewabeba viongozi wetu, ndio wenye kuonyesha mfano mbaya kwa kuendesha kwa kasi barabarani.

Inasikitisha.



Kinachosababisha Ajali Mbaya Kwenye Barabara Zetu.. (2)
- Madereva wengi wanaendesha na pombe vichwani

Ndugu zangu, 

Taifa kwa mara nyingine tena limekumbwa na huzuni kubwa kwa matukio ya ajali. 

Nini hasa kinachangia ajali hizi?

Pamoja na kwamba yeyote yule anaweza kukumbwa na ajali ya bahati mbaya, lakini, ajali nyingi hutokana na uzembe wa madereva.

Nilianza kwa kutaja mwendokasi. Sababu ya pili ni madereva kuendesha wakiwa wamekunywa pombe.

Magari mengine yanayoendeshwa kwenye barabara zetu ni kama makombora ya kuangamiza na kuteketeza roho za watu. 

Ni kwa vile, wenye kuyaendesha magari hayo wana ulevi kwenye damu zao. Kuna madereva wanaokunywa kabla au wakiwa safarini.

Pombe huathiri maamuzi ya dereva awapo barabarani. Pombe hupelekea ajali nyingi.

Wenzetu Ulaya, Marekani na kwingineno, kuna sheria yenye kutoa adhabu kwa dereva atakayekutwa akiendesha na unit za pombe kwenye damu yake zilizozidi kiwango kilichowekwa na taifa husika.

Hapa nyumbani kuna matrIki kadhaa ambao hutumia vifaa maalum vya dereva kupuliza kupima kiwango cha pombe kama kimo kwenye dami yake. 

Vifaa hivi vinapaswa kuongezwa. Lakini, nchi ije na kiwango cha ukomo wa units za pombe kwenye damu kwa aliyekunywa.

Maana yake nini?

Utaratibu huo utaambata na adhabu. Mathalan, dereva atakayekutwa anaendesha huku amekunywa pombe apewe adhabu ya kifungo cha kwenda jela, maana atakuwa ametenda kosa la kusababisha uhai wa raia kupotea.

Kwa sasa tukubali hali ni mbaya kwenye barabara zetu kwa kuwa na baadhi ya madereva wenye kuendesha wakiwa wamekunywa pombe. 

Na unaweza kumkuta dereva anakunywa mpaka saa saba za usiku na kuanza kuendesha gari saa kumi na moja asubuhi. Kimsingi dereva huyo atakuwa anaendesha akiwa amelewa.

Mwenyewe atasema:
" Pombe nimekunywa jana usiku!"

Dereva huyu hajui kuwa pombe mwilini inachukua saa zisizopungua tatu kutoka mwilini baada ya glasi au chupa ya mwisho.

Inasikitisha.
Maggid

No comments:

Post a Comment