MAHAKAMA ya Katiba nchini Uganda imeidhinisha mageuzi ya katiba yaliondoa
kikomo cha umri wa kugombea urais. Awali umri wa kugombea ulikuwa uwe miaka 75
jambo ambalo lingembana Rais wa sasa Yoweri K. Museveni kuomba ridhaa ya
kuchaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo.
Majaji wanne kati ya
watano wa jopo la majaji wamesema mageuzi hayo hayakiuki katiba, na pia hayendi
kinyume na hsri aya muongozo wa bunge nchini.
Awali umri wa mwisho
kwa kugombea ilikuwa miaka 75. Hii ina maana Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta
Museveni atakua huru kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.
Kikao cha kutoa uamuzi
huo uliowasilishwa katika mahakama kuu huko Mbale kilianza kwa naibu jaji mkuu,
Alfonse Owiny-Dollo, kuanza kwa kuomba radhi kwa mahakama kuchelewa kuanza kwa
muda uliopangwa awali.
Hata hivyo mahakama
imekataa kuongeza miaka ya wabunge waliotaka kusalia madarakani kwa miaka 7
badala ya mitano ya sasa.
Katika
uamuzi wake Jaji Cheborion Barishaki ameeleza kwamba kuongezwa kwa muhula wa
kuhudumu bunge kutoka miaka mitano hadi miaka saba itakuwani hatua ya kibinfasi
na inakwenda kinyume na maadili ya uongozi bora:
Ameeleza
kwamba kwa kutowashauri raia kuhusu kuongeza muhula wa kuhudumu, wabunge
wamejilimbikizia uongozi ambao unatolewa kikatiba kwa watu kuamua ni nani
wanaemtaka awaongoze.
Na kwa kuongeza muda wa
wabunge kuhudumu kwa miaka miwili zaidi, viongozi hao wamewanyima raia nafasi
za uchaguzi mwaka 2021, uliopangiwa uchaguzi mkuu nchini.
"Katiba
ni ya kuwatumikia watu na sio kwa namna nyingine yoyote," alisema.
Kesi hii imewasilishwa
baada ya watu kutoridhia hatua ya mageuzi hayo ya katiba yaliokumbwa na mzozo
mwaka jana, yaliochangia kuondolewa kwa kikomo cha umri wa kugombea urais, na
kuongezwa muda wa kuhudumu nyadhifa za kisiasa kutoka miaka mitano hadi misaba.
Raia nchini Uganda
Alhamisi walifuatilia kwa makini uamuzi huo ukipitishwa kutoka mahakama ya
katiba Mable kupitia vyombo vya habari na hata pia mitandao ya kijamii.
Na
wakati uamuzi ukiendelea kusomwa kuhusu kuidhinishwa kwa kikomo cha umir wa
kugombea urais - hatua inayoonekana ambayo huenda ikamruhusu Rais Yoweri
Museveni kuendelea kuhudumu madarakani kwa zaidi ya utawla wake wa miongo
mitatu, haya ndio baadhi ya yaliozungumzwa mitandaoni: Kumekuwa na pingamizi
kwa pendekezo la kuibadili katiba mwaka jana sio tu miongoni mwa raia nchini,
lakini pia upinzani, viongozi wa kidini na hata baadhi ya wafuasi katika chama
tawala Uganda.
Kulishuhudiwa
maandamano makubwa kupinga hatua hiyo katika sehemu tofauti
nchini na kusababisha Polisi kuingilia kati na kujaribu kuzima ghasia
zilizozuka.
-BBC
No comments:
Post a Comment