Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy , akiwa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar – nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kumfariji na kumpa pole kufuatia msiba wa kuondokewa na mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
UPENDO ni hali ya moyo inayomfanya mtu kujali, kuhurumia na kuguswa na hali ya mwingine bila chuki, kinyongo wala ubaguzi. Ni tunu inayojenga utu na mshikamano katika jamii.
Katika maisha ya kila siku, upendo wa kweli hauishii kwenye maneno mazuri, bali huonekana zaidi kupitia matendo, hasa pale mtu anapoweza kusimama na mwenzake katika nyakati za furaha na huzuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, amekuwa akijenga taswira ya kiongozi anayethamini utu, huruma na kujali watu anaowaongoza.
Baadhi ya watumishi anaowaongoza wanaufahamu ubinadamu wake, wakishuhudia namna ambavyo amekuwa karibu nao katika matukio mbalimbali ya kijamii, ikiwemo nyakati za furaha na changamoto.
Ukaribu huo umeendelea kumfanya Mhandisi Saidy kuwa kiongozi anayegusa maisha ya watu, si kwa nafasi yake pekee, bali pia kupitia namna anavyoshirikiana na kuwajali watu wanaomzunguka.
Katika kuonesha kwa vitendo maana ya upendo na mshikamano, Mhandisi Saidy amefika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha majonzi.
Amefika kutoa pole na faraja kufuatia kifo cha mume wa Rais Samia, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026, wakati akipatiwa matibabu.
Hatua hiyo imebeba ujumbe wa kina wa ubinadamu, kwani katika nyakati za majonzi, uwepo wa mtu anayekuja kushiriki huzuni na kutoa faraja unaweza kuwa ishara kubwa ya upendo na mshikamano.
Kwa mtazamo wa kiimani na kijamii, dini mbalimbali zimeendelea kufundisha umuhimu wa upendo, huruma na kuwafariji wenye huzuni. Hivyo, kitendo cha kusimama na mwingine wakati wa majonzi ni sehemu ya utu unaounganisha jamii.
Kwa Mhandisi
Hassan Saidy, kufika Kizimkazi ni zaidi ya ziara; ni ishara kwamba uongozi
unapounganishwa na utu, upendo huonekana katika matendo.
....................
Habari hii imeandikwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.


No comments:
Post a Comment