
Bw. Bakari Steven Machumu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:- 
Bw. Tido Mhando.
Amemteuwa Bw. Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano Ikulu; huku Bw. Bakari Steven Machumu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu. Bw. Machumu anachukua nafasi ya Bi. Sharifa Bakari Nyanga ambaye amepangiwa majukumu mengine;
Wakati huo huo amemteuwa Bw. Lazaro Samuel Nyalandu kuwa Balozi.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka KATIBU MKUU KIONGOZI 19 Novemba, 2025

No comments:
Post a Comment