![]() |
MBUNGE wa Jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu,
amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uchaguzi
huo umefanyika jijini Dodoma ambapo Zungu amepata kura 378 zilizopigwa na
wabunge na kumuwezesha kushika nafasi hiyo muhimu ya kuongoza Bunge la 13 la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
Ushindi huo unampa jukumu la kusimamia shughuli zote za chombo
hicho cha kutunga sheria, kuhakikisha uwajibikaji na kuimarisha utekelezaji wa
majukumu ya Bunge kwa manufaa ya wananchi. Katika uchaguzi huo, wagombea
wengine waliokuwa wakishindana naye ni Veronica Tyeah kutoka Chama cha National
Reconstruction Alliance (NRA) aliyepata kura 0, Anitha Mgaya wa National League
for Democracy (NLD) kura 0, Chrisant Nyakitita wa Democratic Party (DP) kura 0,
Ndonge Ndonge wa Alliance for Africa Farms Party (AAFP) aliyepata kura 1, na
Amin Yango wa Alliance for Democratic Change (ADC) aliyepata kura 1. |



No comments:
Post a Comment