PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI ATEMBELEA BANDA LA WAKALA WA VIPIMO NANENANE NA KUWAPONGEZA KWA KAZI NZURI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 7 August 2025

PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI ATEMBELEA BANDA LA WAKALA WA VIPIMO NANENANE NA KUWAPONGEZA KWA KAZI NZURI



WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho ya NaneNane Dodoma na kuwapongeza watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mhe. Kabudi amesema WMA ni miongoni mwa Taasisi muhimu za Serikali zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. 

Ametoa rai kwa watendaji wa WMA kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuwalinda walaji katika sekta zote nchini wakiwemo wakulima kupitia jukumu lao kuu la uhakiki wa vipimo.

No comments:

Post a Comment