AFISA MTENDAJI MKUU DSE AJITAMBULISHA KWA WAZIRI WA FEDHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 3 September 2024

AFISA MTENDAJI MKUU DSE AJITAMBULISHA KWA WAZIRI WA FEDHA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza kuhusu maendeleo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), alipokutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza mkutano kati yake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Bw. Peter Nalitolela, aliyefika kujitambulisha, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Na Peter Haule, WF, Dodoma

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salam (DSE) aliyefika kujitambulisha.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Dkt. Nchemba, jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment