WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amemuaga Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing – Spandet baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri Makamba amempongeza Balozi Mette kwa kazi nzuri aliyoifanya nchini katika kipindi cha uwakili wake, sio tu kwa kukuza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Denmark vilevile kwa mchango wake hadhimu kwenye utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ambayo imechangia katika ukuaji wa maendeleo nchini.
Aidha Waziri Makamba amempongeza Balozi Mette kwa mchango wake alioutoa katika kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya TabiaNchi na masuala ya amani na usalama.
Kwa upande wake Balozi Mette ameeleza kuwa licha kuendelea kukua kwa uhusiano wa kidiplomasia bado juhudi zaidi zinahitajika katika kukuza kiwango cha biashara na uwekezaji katika ya Tanzania na Denmark. Aidha, Balozi Mette ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote akitimza majukumu yake hapa nchini.
Natambua kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, licha kumaliza kipindi changu cha kuhudumu kama Balozi, nitaendelea kutoa mchango wangu kwa namna mbalimbali ili kuhakikisha kiwango cha biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Denmark kinaongezeka.
Alieleza Balozi Mette
Tanzania na Denmark zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, elimu na biashara na uwekezaji.
No comments:
Post a Comment