KASEKENYA AAGIZA KUWEKWA ALAMA ZA TAHADHARI MLIMA BUSUNZU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 16 June 2024

KASEKENYA AAGIZA KUWEKWA ALAMA ZA TAHADHARI MLIMA BUSUNZU

 

Muonekano wa daraja la Malagarasi lenye urefu wa mita 77, mkoani Kigoma. Daraja hilo limejengwa na mkandarasi STECOL na limekamilika kwa asilimia 100.

Muonekano wa barabara Kabingo - Kasulu – Manyovu (Km 260) sehemu ya Mvugwe – Nduta (Km 59.35), mkoani Kigoma. Barabara hiyo inajengwa na mkandarasi STECOL kwa gharama ya shilingi Bilioni 84 na inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2024.

Muonekano wa kipande cha barabara kilichoharibika chenye urefu wa takriban mita 100 eneo la mlima Busunzu, mkoani Kigoma. Mkandarasi STECOL anasubiri timu ya wataalam inayotafiti eneo hilo kupata utatuzi wa kudumu ili kuendelea na ujenzi katika kipande hicho.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya (Wakwanza kushoto) wakati alipokagua maendeleo ya miradi ya barabara mkoani humo.

Mhandisi, Hamisi Juma kutoka Kampuni ya Mhandisi Mshauri M/s Conseil Ingenierie Limited (CIRA SAS) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya (Wakwanza kushoto) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kabingo - Kasulu – Manyovu (Km 260) sehemu ya Mvugwe – Nduta (Km 59.35), mkoani Kigoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kigoma, Eng. Narcis Choma (Wapili kushoto mbele), alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kabingo - Kasulu – Manyovu (Km 260) sehemu ya Mvugwe – Nduta (Km 59.35), mkoani humo.

No comments:

Post a Comment