| Wakristo wameambiwa Jumatano ya Majivu , wanapakwa majivu kama ishara ya toba |
Wakristo wameambiwa Jumatano ya
Majivu , wanapakwa majivu kama ishara ya toba na katika kipindi hi Ki wanatakiwa
kusafiri katika unyofu wa moyoni.
Hayo yamesemwa katika Kanisa la
Bikira Maria Malkia wa Wamisionari , Parokia ya Malya , Jimbo Kuu Katoliki la
Mwanza na Padri Samson Masanja katika misa ya Jumatano ya Majivu iliyoanza saa
9 alasiri na kumaliza saa 11 jioni ya Jumatano ya Februari 14, 2024.
Padri Masanja aliongeza kuwa
“Kila Mkristo anatakiwa kujiweka mikononi
mwa Mungu, kukumbuka sana kusoma neno la Mungu na pia kuyafanya matendo ya
huruma kwa wahitaji.”
Akihitimisha misa hiyo, Padri Masanja
alikumbusha waamini hao kukumbuka kuwa Jumapili ijayo ya Februari 18, 2024 kila
Kigango cha Parokia ya Malya kutakuwa na zoezi na uwezeshaji (Kuwategemeza ) makatekista
maana wao ni walimu wanaotoa mafundisho ya kiroho katika kila kigango, hivyo
waamini wote aliomba wajiandae
Wakati misa hiyo inafanyika, hali ya
hewa ya Malya ilikuwa na ngurumo za hapa na pale, manyunyu kidogo na joto kali,
huku kanisa hilo likijaa waamini wengi ambapo umati mkubwa ulijaza ndani ya
kanisa, nalo kundi kubwa la pili la waamini likiujaza pia uwanja kando ya
kanisa hili .
Kutokana na umati huo mkubwa, zoezi
la kupakwa majibu liliendelea na makatekista wawili mara baada ya misa
kumalizika, nia ni kutoa nafasi kwa waamini ambao walichelewa kupakwa majivu
awali.
Mandhari ya kiwanja cha kanisa hilo
ilipambwa na misururu mirefu ya waamini wa rika zote, wakijongea katika lango
la kanisa hilo na makatekista hao wawili mama na baba walisimama katika ngazi
za lango kuu la kanisa na kuwapaka majivu.
Wakati misa hiyo inaanza hadi
inamalizikia pembezoni mwa kanisa hili ilisikika sauti ya jenereta ikiunguruma
ambapo ilitumika kufua umeme uliotumika kutoa mwanga kanisa hapo maana kwa
mchana mzima ya Februari 14, 2024 eneo lote la Malya halikuwa na umeme kwani
ulikatika asubuhi na kurudi saa 12, 00 jioni.

No comments:
Post a Comment