Na
Mwandishi Wetu, Morogoro
Imeelezwa
kuwa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la mto Ruaha Mkuu lililopo kwenye barabara ya
Kidatu – Ifakara lenye urefu wa mita 133 mkoani Morogoro, utakapokamilika utakuwa
na manufaa makubwa ikiwemo kuchagiza maendeleo, kukuza uchumi pamoja na
kuunganisha mkoa huo na Mikoa mingine ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi na
Mtwara na nchi jirani.
Akizungumza
hivi karibuni Kaimu Mhandisi Mkazi wa Mradi huo unaokwenda sambamba na ujenzi
wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 66.9 kiwango cha lami, Mhandisi Marcel
Kiimu amesema katika daraja hilo magari yatapita mawili ikiwa ni moja kila
upande, tofauti na awali yalipita moja kwani ni jembamba hivyo limesababisha msongamano
wa magari.
Amesema
pia kwenye barabara hiyo kumejengwa kumejengwa madaraja mengine ya kawaida
manne ambayo ni Ikela, Msolwa, Sumbugulu na Kisawasawa, makalavati makubwa 45
yenye urefu wa mita 584 kwa kila moja na makalvati ya kawaida 249, ambayo yote yatasaidia
kupitisha maji kwa haraka.
Mradi
huo wa kimkakati ni sehemu ya mkakati wa Taifa wa kuwasaidia wakulima wadogo wanaolima
mazao ya chakula na biashara kupitia Programu ya uendelezaji Kilimo katika Ukanda
wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), waliopo katika Bonde la Mto Kilombero, Ulanga,
Mlimba na Malinyi.
Amesema
barabara hiyo itakuwa na upana wa mita 9.5 ikiwa ni njia ya magari yenye upana
wa mita 6.5 yenye lami nzito (asphalt concrete) na mabega ya barabara yenye
upana wa mita 1.5 kwa kila upande wa maeneo yasiyokuwa na miji na upana wa mita
2.0 kila upande wenye miji, mitaro ya kupitisha maji na vivuko vya watembea kwa
miguu.
Mha.
Kiimu ameongeza kuwa mradi huo ujenzi wa barabara ya Kidatu- Ifakara unaotarajiwa kukamilika
Machi 2024 unasimamiwa na Kitengo cha TECU cha Wakala ya Barabara Tanzania
(TANROADS), ambapo utatumia gharama ya zaidi ya Shilingi Bil. 128.15, unawafanyakazi
792 kati yao wazawa ni 779 na 13 ni wageni, miongoni mwao wanaume ni 703 na
wanawake ni 89. Pia kuna wahandisi wahitimu wa vyuo vikuu watano na wanafunzi
toka vyuo vikuu saba.
No comments:
Post a Comment