TANZANIA NA IVORY COAST KUSAINI “MOU” SEKTA YA MICHEZO - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Friday, 26 January 2024

demo-image

TANZANIA NA IVORY COAST KUSAINI “MOU” SEKTA YA MICHEZO

0M3A0174

0M3A0190

0M3A0263

Na Brown Jonas, Abidjan*

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Januari 26, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast Mhe. Adjé silas ambapo katika mazungumzo yao wamejadili juu ya kusaini makubaliano maalum ya ushirikiano (MOU) katika sekta ya michezo baina ya nchi hizo ili kuibua na kukuza vipaji.

Mhe. Ndumbaro ameipongeza nchi hiyo kwa maandalizi mazuri ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayoendelea kwa kujenga miundombinu mizuri ikiwemo viwanja na barabara.

Amesema Tanzania inajifunza kwa Ivory Coast kwa kuwa itakua mwenyeji wa michuano hiyo kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Tanzania Bw. Ally Mayai  na viongozi wengine wa Wizara ya Michezo wa Ivory Coast.
Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *