BASHUNGWA AITAKA TANROADS KUPANDA NA KUHUDUMIA MITI KATIKA MAENEO YA BARABARA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 29 January 2024

BASHUNGWA AITAKA TANROADS KUPANDA NA KUHUDUMIA MITI KATIKA MAENEO YA BARABARA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akipanda mti wa Mwembe wakati akiongoza Watumishi wa Wizara katika zoezi la upandaji miti kwenye eneo la Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Januari 29, 2024.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akimwagilia mti wa Mwembe wakati akiongoza Watumishi wa Wizara katika zoezi la upandaji miti kwenye eneo la Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Januari 29, 2024.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, akipanda mti wa Stafeli wakati wa zoezi la upandaji miti kwenye eneo la Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Januari 29, 2024.

Sehemu ya Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi, ikishiriki zoezi la upandaji wa miti kwenye eneo la Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Januari 29, 2024.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ujenzi wakishiriki zoezi la upandaji wa miti kwenye eneo la Wizara Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Januari 29, 2024.

Muonekano wa juu wa Ofisi mbalimbali za Wizara na barabara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma zilizopendezeshwa kwa kupandwa miti mbalimbali ya Kivuli na Matunda.

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuendelea kupanda na kuhudumia miti iliyopandwa katika maeneo ya barabara kwa ajili ya kuendelea kupendezesha miji na kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Bashungwa amezungumza hayo katika Ofisi za Wizara zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma Januari 29, 2024 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kwa ajili ya kuendeleza kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Ameitaka TANROADS kuhakikisha inaendelea kuhudumia miti walioipanda katika barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver (km 10), jijini Dodoma na kuwasisitiza kurudishia miti iliyokufa ili kuendelea kuboresha na kupendezesha eneo hilo.

“Hakikisheni TANROADS mnaihudumia miti mliyoipanda katika barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver (km 10), mnaiangalia kwa ukaribu na kupanda miti mipya kwa ile iliyokufa kama mlivyoelekezwa na Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango”, amesema Bashungwa.

Bashungwa ametoa wito kwa watanzania kuendelea na tabia ya kupanda miti na wasisubiri kupewa maagizo kutoka kwa viongozi wakuu wa Serikali.

“Tabia ya kupanda miti iwe ni ya hiyari, tusisubiri hadi viongozi wakuu kusisitiza kufanya hivyo muendele na tabia hii hata majumbani kwenu, ikiwa mti utakufa basi rudishieni mti mwingine tena”, amesema Bashungwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Mhandisi Aisha Amour, amesema kuwa zoezili hilo limeshirikisha upandaji wa miti tofauti zaidi ya 100 ikiwemo miti ya matunda na kivuli.

Balozi Aisha ameahidi kuendelea kuitunza miti hiyo na kuongeza miti mingine zaidi ili kuendelea kuifanya Ofisi hiyo kuwa ya kijani.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi


No comments:

Post a Comment