Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Jorodom ambalo
limeathirika na Mafuriko pamoja na
maporomoko ya matope na mawe Wilayani Hanang Mkoani Manyara tarehe 7
Desemba, 2023. Rais Samia alijionea uharibifu mkubwa uliotokea na kuwapa pole
Waathirika wa maafa hayo na kuwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao.
 |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.
Queen Sendiga akielezea kuhusiana na athari za mafuriko yaliyotokea katika eneo
la Jorodom Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia ametembelea eneo hilo Mkoani
Manyara tarehe 7 Desemba, 2023 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ndugu Elibariki Naman mkazi wa Jorodom, Katesh
ambaye ni muathirika wa Mafuriko yaliyotokea Wilayani Hanang. Ndugu Elibariki
alikuwa akielezea jinsi majirani zake walivyopoteza maisha pamoja na makazi yao
katika maafa hayo
 |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji muathirika wa mafuriko
yaliyotokea Katesh Bi. Salome Elifuraha ambaye amelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Tumaini iliyopo Katesh, Hanang. Mama amepoteza watoto wawili kwenye
maafa hayo huku mtoto wa tatu akiwa bado hajapatikana hadi sasa. Rais Samia
aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo |
No comments:
Post a Comment