KATIBU MKUU MSIGWA AMPONGEZA MOTELA KUCHAGULIWA KUWA KATIBU WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 17 November 2023

KATIBU MKUU MSIGWA AMPONGEZA MOTELA KUCHAGULIWA KUWA KATIBU WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA



Na Eleuteri Mangi, WUSM

BARAZA la Wafanyakazi Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kauli moja wamemchagua Sephania Motela kuwa Katibu wa Baraza hilo kwa kura 19 kati za wajumbe 36 waliopiga kura chini ya Mwenyekiti wa Baraza la na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Gerson Msigwa.

Uchaguzi huo umefanyika Novemba 16, 2023 wakati wa Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika jijini Dodoma na kusimamiwa na Bi. Neema Dickson kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. Msigwa amempongeza Bw. Sephania Motela kwa kuchaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Bw. Bernard Lobogo ambaye ameteuliwa kuwa  Mkuu wa Kitengo kipya cha Tathmini na Ufuatiliaji katika Wizara hiyo.

Akiwashukuru wajumbe kwa kumpa dhamana hiyo, Bw. Motela amewashukuru wajumbe hao kwa kumwamini kuchagua katika nafasi hiyo na kuahidi kufanyakazi kwa moyo kwa kushirikiana na Menejimenti ili kufikia matarajio ya Wizara.

"Tutafanya kazi kama timu ili wizara iendelee kuakisi Jina lake la kuwa wizara ya kuwaletea furaha Watanzania" amesema Bw. Motela.

Mkutano huo ni wa kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo kwa mwaka inatakiwa kufanyika mikutano miwili kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment