KUITIKA HAKUTOSHI BILA MATENDO-PADRI MASANJA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 1 October 2023

KUITIKA HAKUTOSHI BILA MATENDO-PADRI MASANJA



Na Adeladius Makwega-MWANZA

WAKRISTO wameambiwa kuwa Mungu umtafuta mwanadamu hata katika nyakati za mwisho, kwa hiyo mwanadamu hapaswi kukata tamaa kwa kuwa yeye ni mdhambi, bali abadilishe mwenendo wake na kufanya mabadiliko hayo kwa matendo na si maneno.


Hayo yamesemwa katika misa ya Kwanza ya Dominika ya 26 ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa, Katika Kanisa la Bikira Maria Malkia wa Wamisionari na Padri Samson Masanja,  Paroko wa Parokia ya Malya-  Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.


‘Katika Injili ya ya dominika hii(Mt 21:28-32) inasisitiza kuwa maisha ya mwanadamu kuitika kwake katika mambo mbalimbali hakutoshi, bali daima anatakiwa kutenda. Leo tunaungama imani yetu kwa kumuamini Kristo, haya maneno hayatoshi, bali yanatakiwa kusindikizwa na matendo yetu. Je kweli katika mazingira yetu sisi ni Wakrsto wa matendo au maneno? Ndiyo maana injili inaonesha kijana aliyekata-  alitenda na yule aliyekubali -hakutenda, tubadili mwendo  wetu.’


Padri  Masanja alisisitiza kuwa kila Mkristo aibebe fadhili ya unyenyekuvu katika maisha yake ambapo Yesu Kristo mwenyewe alibeba fadhili hii hadi kuja kutukomboa.


Misa hiyo ilivyofanyika katika hali ya utulivu mkubwa huku kukiwa na baridi kwa mbali, jua likichelewa kutoa miale yake,  iliambatana na nia na maombi kadhaa,


‘Tunaomba kwa ajili ya viongozi wa dini na serikali, watambue kuwa hakuna maendeleo na ustawi wa nchi, bila ya kuwajibika, Eee Bwana -Twakuomba utusikie.’


Hadi misa hiyo ya kwanza inamalizika hali ya hewa  ya eneo zima la Malya na viunga vyake ilikuwa ya vipindi vya jua, mawingu kidogo na mvua kidogo nyakati za jioni.


 Mandhari ya mashamba mengi kwa sasa ni matrekta yakiunguruma, ng’ombe wakikokota majembe kulima, huku kazi hiyo ikisindikizwa na miluzi na ishara za wanaowaongoza wanyama hao, nyuma ya wanyama na matrekta hayo wakulima wakifuata nyuma ya matrekta na wanyama hao wakipanda mazao mbalimbali.


No comments:

Post a Comment