JE, NI KWELI SHERIA INATAKA GARI ZA ABIRIA ZIWE NA GAVANA PEKEE KAMA KIDHIBITI MWENDO?
Jibu ni la hasha.
Kifungu cha 51 cha sheria ya usalama barabarani Tanzania ndicho kinachozungumzia masuala ya mwendokasi, upimaji wake, adhabu na udhibiti wake. Kifungu cha 51(5) kinasema hivi(Kwa kiingereza):
“No person shall drive a public service vehicle other than a taxi-cab on a public road, unless that vehicle is fitted with a speed governor or any other similar device designed to regulate and or record the speed of that vehicle”.
Tafsiri ya kifungu hicho ni nini?
Tafsiri ya kifungu hicho ni kwamba “Hairuhusiwi kwa mtu kuendesha gari la abiria isipokuwa teksi katika barabara za umma, isipokuwa kama gari hilo limefungwa spidi gavana au kifaa kinachofanana na hicho kwaajili ya kudhibiti mwendo na au kurekodi spidi ya gari hilo”.
Hii ina maana gani?
Ili tuweze kupata maana halisi ya kifungu hiki, yatupasa kukitafsiri(interpret) kwa kukichambua kwa kukigawa katika viini vyake kama ifuatavyo
(a)No person shall driver a public service vehicle other than a taxi cab on a public road
(Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuendesha gari la abiria barabarani isipokuwa teksi.) Maana yake hapa ni kwamba magari yanayohusika na kifungu hiki ni yale yote ya abiria isipokuwa yanayofanya huduma za teksi.
(b)Unless that vehicle is fitted with
(Isipokuwa kama gari hilo limefungwa)
(c)A speed governor or;
(Spidi gavana)
Yaani hapa sharti la kwanza gari hilo liwe limefungwa spidi gavana au kama halina spidi gavana
(d)Any other similar device
Liwe na kifaa chenye kufanana na spidi gavana
(e)Designed to regulate and or record the speed of that vehicle
Kilichotengenezwa kwaajili ya kudhibiti na au kurekodi mwendo wa gari hilo.
Hii ina maana kwamba gari linaweza lisiwe na spidi gavana ila likawa na kifaa kingine chochote kinachofanana na spidi gavana chenye:
(aa) uwezo wa kudhibiti mwendo na kurekodi mwendo wa gari hilo au
(bb) uwezo wa kudhibiti au kurekodi mwendo wa gari hilo.
Hii inatupa picha kwamba sio lazima gari liwe na spidi gavana bali linaweza kuwa na kifaa kingine chochote cha kudhibiti na kurekodi mwendo au kurekodi mwendo. Kwani neno and/or linamanisha kimojawapo au vyote viwili, Yaani kama kuna vitu A na B, basi yakitumika maneno “A and/or B” maana yake ni Kitu A au kitu B au vyote kwa pamoja. Angalia inavyosemwa hapa (And/or, however, is not ambiguous at all. It has a definite, agreed-upon meaning: when used properly, the construct means “A or B or both.” In most areas of law, there simply is no compelling reason to avoid using and/or. The term is clear and concise. It derives criticism mainly from the inability of people to use it correctly.)
Kwa lugha nyingine gari inaweza kuwa na gavana au kifaa kingine chochote kama vile VTS ambacho kinaweza kutumika kudhibiti mwendo na kurekodi au kurekodi pekee.
Ni imani yangu makala hii itasaidia kujenga uelewa na kuibua mjadala pia.
RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote
No comments:
Post a Comment