Dotto Mwaibale na Thobias Mwanakatwe, Hanang
WANANCHI wa vijiji vya Gaghata,Nyabat na Bassodesh kata ya Bassodesh,
wilayani Hanang' mkoani Manyara wamemliilia
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo wakimuomba aingilie kati kutokana na kuchukuiwa mashamba yao mashamba yao zaidi
ya ekari 1000 ambayo amepewa mwekezaji ambaye ameshindwa kuyaendeleza na
kusababisha wakose maeneo ya kulima na kufugia mifugo yao ..
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti ambao walifika
katika vijiji hivyo, walisema maeneo hayo alipewa mwekezaji wa ambaye ni Hospitali ya Hydom (Hydom Lutheran
Hospital) inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) na
viongozi wa kijiji hicho tangu mwaka 1992 lakini hayaendelezwi na badala yake
wamekuwa wakiyakodisha.
Walisema wamelazimika kumuomba Chongolo aingilie kati mgogoro huo ambao
umedumu kwa zaidi ya miaka 30 bila kupatiwa ufumbuzi ambapo viongozi wa wilaya
hiyo mwishoni mwa mwezi wa Februari, 2023 walilazimika kwenda katika kijiji cha
Basidosh kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho baada ya vyombo vya habari
kuibua sakata hilo hilo baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo, Qwari Sulle
kulalamika ngazi ya juu kufuatia eneo lake alililoachiwa na baba yake aliyekuwa
akilimiliki tangu mwaka 1979 kabla ya mwekezaji huyo kufika mwaka 1992..
Walisema katika hali ya kushangaza kila wanapokwenda kulalamikia haki yao
katika ngazi nyingine za serikali baadhi ya viongozi wakiwamo wanasiasa
wastaafu ambao wanatajwa kuhusika katika mgogoro huo baada ya kumpa mwekezaji
huyo wamekuwa wakitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambao huenda kuwakamata na
kuwaweka ndani hasa mwananchi ambaye ameonekana kuwa mstari wa mbele kufuatilia
suala hilo na tayari mapema mwezi huu amepelekwa mahakamani na kufunguliwa kesi
ya jinai.
Mapema mwezi uliopita mwananchi Qwari
Sulle alipata kadhia ya kukamatwa na polisi wa kituo cha Bassotu na baadaye
kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Hanang' ambako alilala huko hadi siku ya pili
alipoachiwa kwa kujidhamini mwenyewe na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Katabazi kuthibitisha tukio hilo.
Sulle ambaye eneo lake la ardhi la ekari 32 ambazo anadai zimechuliwa na
mwekezaji huyo inaelezwa aliwekwa ndani kituo cha polisi kwa kile kilichoelezwa
kuwa ni agizo kutoka kwa kigogo mmoja wa serikali wilayani kufuatilia kiongozi
mmoja wa kisiasa mstaafu kulalamika kuwa
mwananchi huyo aliwapeleka wanahabari kijijini hapo.
Sulle alisema mwishoni mwa Desemba mwaka jana alikwenda kupeleka malamiko
yake kwa Mkuu wa Wilaya Hanang’, Janeth Mayanja ambaye alimtaka aandike barua
ya malamiko ambayo aliiandika na kumkabidhi Katibu Tawala wa wilaya hiyo John
Bura kama alivyoagizwa na mkuu wa wilaya lakini kila alipokuwa akienda kuulizia
hakupewa majibu yoyote ndipo alipoamua kwenda ngazi nyingine na kwa vyombo vya
habari kulalamika jambo lililouibua uongozi wa wilaya hiyo na kufika kijijini hapo.
Mbali ya Sulle kulalamikia jambo hilo linalohusu eneo lake la ekari 32
zilizochukuliwa na mwekezaji huyo wananchi wa vijiji hivyo wamekuwa
wakifuatilia jambo hilo tangu mwaka 1990 ambapo Oktoba 15, 2012 waliandika
barua katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Hanang' kuomba wasaidiwe
suala hilo lakini hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana.
"Mwekezaji huyu wakati anapewa mashamba hayo mwaka 1992 yaliwekwa
makubaliano kati ya serikali ya vijiji hivyo ambavyo awali kilikuwa ni kijiji
kimoja cha Basodesh kuwa awajengee lambo la kunyweshea mifugo, wajengewe
zahanati na shule lakini hadi leo hii ni miaka 30 imepita hajatekeleza
makubaliano na wala kuyaendeleza mashamba hayo ambayo sehemu kubwa ni msitu na
hata hayo yanayolimwa ni yale yanayokodishwa kwa wananchi na hospitali
hiyo" alisema mmoja wa wananchi hao.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Basodesh, Patrick
Amo akizungumza katika mkutano huo wa utatuzi wa mgogoro huo uliotwishwa na
mkuu wa wilaya hiyo alisema hospitali hiyo imepoteza sifa ya kumiliki mashamba
hayo kutokana na kushindwa kutekeleza makubaliano na kuyaendeleza mashamba hayo
kwa zaidi ya miaka 30.
Amo aliongeza kuwa kutokana na kuongezeka kwa watu na ardhi kuwa ndogo na
mwekezaji huyo kuwa na ardhi kubwa ambayo haiendelezi alimuomba mkuu wa wilaya
hiyo kuangalia namna bora ya kutatua mgogoro huo.
Aidha, Amo alimuomba mkuu wa wilaya kuangalia namna ya kumsaidia eneo mzee
Sulle Tlehhema ambaye aliahidiwa na serikali ya kijiji kuwa angepewa eneo
lingine baada ya lile alilokuwa akilitumia kwa malisho ya mifugo YAKE na kilimo
kupewa mwekezaji.
Alisema hivi sasa kijiji hicho hakina ardhi hivyo kama itafaa hospitali
hiyo ikate sehemu na kumuachia mzee huyo ekari hizo 32 alizompa mtoto wake
Qwari ambazo zipo mpakani mwa shamba hilo na kijiji kingine.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Taghata Nestory John alisema mgogoro huo ambao
umedumu kwa muda mrefu umesababisha wananchi kukataa misaada inayotolewa na
hospitali hiyo kama kujenga ofisi ya kijiji wakidai ni danganya toto kwa kuwa
imechukua ardhi kubwa na kuwaacha wananchi wakiwa hawana mashamba wala maeneo
ya kilimo.
Katibu wa CCM Kata ya Basodesh, Paul Silaa alisema mgogoro huo sio mkubwa
kwa kiasi hicho ambapo alimuomba mkuu wa wilaya hiyo kuona namna ya kumsaidia
mzee Tlehhema kupata eneo aliloahidiwa na serikali ya kijiji hicho wa wakati
huo pamoja na mama Katelina Salimee ambaye naye alikuwa na ekari 20 ambazo
zimechukuliwa na hospitali hiyo.
Mzee Sulle Tlehhema baba mzazi wa Qwari mwenye umri wa miaka 110
akizungumza kwenye mkutano huo alisema alifika kwenye eneo hilo mwaka 1979 na
kulikuwa na watu wa kuhesabu na mwaka 1992 ndipo alipofika mwekezaji huyo na
hata walipokuwa wakichonga barabara za kuweka mipaka alikuwepo katika eneo
hilo.
Mzee Tlehhma alisema wakati walipokuwa wakiweka mipaka hiyo alipowauliza
viongozi wa kijiji wa wakati huo akiwepo katibu kata mzee Elisha walimuambia
watamtafutia eneo lingine mbadala na hilo na kuwa hadi leo hii kijiji hicho hakijampatia
eneo lolote na hajui hatima yake ni nini
na anaumia sana anapoona mtoto wake akipata misukosuko ya kukamatwa bila ya
kujua aende akaishi wapi na familia yake pamoja na mifugo.
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Hanang', Janeth Mayanja ,
ambaye aliambatana na baadhi ya wataalamu kutoka katika ofisi yake na wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama akitangulia kuvilaumu vyombo vya habari kwa
kutoa taarifa ya mgogo huo alisema mashamba hayo mmiliki halali ni hospitali
hiyo.
"Kwa mujibu wa vielelezo nilivyonavyo mmiliki wa mashamba hayo ni
Hospitali ya Hydom na wameyapata kwa kufuata taratibu zote na kuna muhutasari
wa makubaliano kati ya serikali ya kijiji wakati huo na wanahati ya kumiliki
mashamba hayo iliyotolewa na wizara ya ardhi miaka 2000" alisema Mayanja.
Mayanja alisema anaipongeza hospitali hiyo kwa kuweka utaratibu mzuri wa
kuwapatia wananchi mashamba hayo kwa ajili ya kuyalima kwa kufuata utaratibu wa
kuandika majina yao.
Hata hivyo, alimshukia mwekezaji kwamba kitendo cha kuwakodisha mashamba
wananchi kinazidisha vurugu.
Aidha Mayanja aliomba mwekezaji huyo aongezewe muda zaidi wa kutekeleza makubaliano aliyotakiwa kuyatekeleza tangu mwaka 1992 ya kujenga lambo, zahanati na shule na aliwaomba wafanya haraka nawananchi waendelee kuwa na imani na mwekezaji huyo na kuanza kupokea misaada yake ikiwemo ya miradi ya maendeleokama kuchimbiwa visima vya maji na kujengewa ofisi ya kijiji na kwa kutofanya hivyo ni kujicheleweshea maendeleo yao.
Ni moja ya shamba ambalo lilikuwa lake ambalo amelima mahindi ili kujikimu na njaa lakini limesababisha kukamatwa na polisi akidaiwa kulilima kinyume na utaratibu na kufunguliwa kesi ya jinai.
|
No comments:
Post a Comment