Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila (kushoto) akiteta jambo na mmoja wa wabunge mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea BRT II. |
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya miundombinu inayosimamiwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), na kuitaka taasisi hiyo kuwasimamia kikamilifu wakandarasi ili waweze kukamilisha kazi zao kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso alipokuwa akitembelea na kushuhudia maendeleo ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka awamu ya pili, 'BRT II' ambao umeanzia Makutano ya Barabara ya Bandari hadi Mbagala ilipo Karakana ya Mabasi hayo.
Mhe. Kakoso amepongeza ujenzi wa barabara za juu katika mradi huo kwani umejengwa vizuri hivyo kuishauri TANROADS kuhakikisha maendeo ya chini ya madaraja hayo yaliowazi yajengewe uzio ili wananchi wasiyatumie vibaya kwani kwa sasa yapo wazi.
"...Nimefuraishwa sana na barabara za juu ulizojenga katika mradi huu, lakini nashauri maeneo yale ya chini myajengee uzio ili yasibaki wazi kwani baadhi ya wananchi wanaweza kuyatumia vibaya," alisema Mhe. Kakoso.
Kwa uapande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kutembelea mradi huo, alisema wizara yake imepokea ushauri na maelekezo ya wajumbe wa kamati hiyo na utahakikisha unayafanyia kazi yote.
Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya BRT II kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya BUNGE ya Miundombinu ilipotembelea Makao Makuu ya TANROADS, Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Eng. Rogatus Mativila alisema hadi sasa ujenzi wa BRT II umefikia asilimia 89.9 ukilinganisha na asilimia 50.1 kipindi kama hiki mwaka jana wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo.
"...Awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu
inahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 20.3 kutoka katikati ya
jiji hadi Mbagala; barabara za juu mbili, daraja moja juu ya reli, daraja moja
la waenda kwa miguu, karakana moja na vituo vya mabasi," alisema Mtendaji
Mkuu wa taasisi hiyo, Eng. Rogatus Mativila.
Imetolewa
na Kitengo cha Habari na Mawasilino Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).
No comments:
Post a Comment