TUNDU LISSU AWASILI TANZANIA TENA, WANACHAMA WAMPOKEA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 25 January 2023

TUNDU LISSU AWASILI TANZANIA TENA, WANACHAMA WAMPOKEA...!

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema - Tundu Antipasi Lissu akiwasili.

Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema - Tundu Antipasi Lissu ukiongozwa na Jeshi la Polisi.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema - Tundu Antipasi Lissu amewasili leo Januari 25, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Ubelgiji na kupokewa na viongozi na wanachama mbalimbali wa Chadema.

Lissu baada ya kuwasili nje ya Uwanja wa Ndege amepokewa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya lango hilo wakiimba na kucheza. Baadaye kiongozi huyo alizungumza na wanachadema katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment