MTANDAO WA WANAHABARI KUTETEA UHAI NA FAMILIA TANZANIA, JOLIFA TZ ‘WAZINDULIWA’ - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 21 December 2022

MTANDAO WA WANAHABARI KUTETEA UHAI NA FAMILIA TANZANIA, JOLIFA TZ ‘WAZINDULIWA’

Baadhi ya wanahabari wa Mtandao wa Jolifa wakiwa Katika picha ya Pamoja na Mlezi wa Mtandao huo, Emil Hagamu ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Uhai Tanzania, Pro-life Tanzania.

Na Frida Manga 

MTANAO wa Waandishi wa Habari za Uhai na Familia Tanzania, (Jolifa Tz) umelenga kutumia Taaluma ya Uandishi na Utangazaji kulinda na kutetea Uhai, Ndoa na familia dhidi ya utamaduni wa kifo.

Mwenyekiti wa Mtandao huo Gaudence Hyera aliyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa awali wa Mtandao huo unaojumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania.

Hyera alisema Jolifa Tz ni asasi isiyo ya kibiashara wala kiserikali na isiyo ya kidini inayojumuisha madhehebu yote ya dini, tayari imeanzisha jukwaa katika Intaneti na mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram nk.

Uzinduzi huo ulikwenda sanjari na Warsha fupi kwa Wanahabari ambapo Mkurugenzi wa Shirika la Utetezi wa Uhai(Pro- Life Tanzania), Emil Hagamu alitoa mada kuhusu thamani ya Uhai na nafasi waliyonayo wanahabari katika kulinda na Kutetea Uhai.

Hagamu alisema Vyombo vya Habari kupitia Wanahabari wanayonafasi kubwa ya kuelimisha Umma kuhusu madhara ya Matumzi ya Vithibiti Mimba na kusaidia kulinda Uhai ambao kwa nyakati za sasa uko kwenye tishio la kupotea.

"Pazeni sauti zenu kupitia taaluma yenu, kuhusu mambo maovu yanayoendelea duniani na pia yanatishia Uhai, pazeni sauti juu ya kushamiri kwa Mapenzi ya jinsi moja, uhamasishaji wa matumizi ya Vithibiti Mimba na Utoaji Mimba, Alisema Hagamu.

" Jueni kwamba ukiruhusu utoaji mimba ujue unajenga roho ya mauaji kwa watoto pia unapandikiza Roho ya chuki na ukatili kwa watoto Waliozaliwa” Alisisistiza.

Aidha Hagamu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kutetea Uhai la Human Life International  (HLI), Kanda ya Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, ametoa rai kwa  viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali nchini kuongeza kasi ya  kukemea kwa sauti Moja juu ya mambo maovu yaliyokinyume na Mpango wa Mungu kwa mwanadamu kama vile matumizi ya vidhibiti mimba, utoaji mimba, mauaji, ushoga, mapenzi na ndoa kwa watu wa jinsi moja.

Mtandao wa Jolifa tz uko ambao uko chini ya Pro- Life Tanzania. ulianzishwa kwa msukumo wa waandishi wanaopenda na kuthamini Uhai na Familia kwa malengo ya  Kulinda utakatifu wa uhai wa binadamu tangu kutungwa mimba hadi kifo chake cha kawaida.

Malengo mengine ni kudumisha Utakatifu wa Ndoa na Familia, Kukuza Utamaduni wa Uhai dhidi ya utamaduni wa kifo, Kulinda thamani ya Uhai wa Binadamu kwa kupinga mitazamo na matendo yanayodhalilisha na kuharibu Utu wa binadamu.

No comments:

Post a Comment