MAGARI SASA RUKSA KUPITA JUU MAKUTANO YA UHASIBU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 30 December 2022

MAGARI SASA RUKSA KUPITA JUU MAKUTANO YA UHASIBU

 

Muonekano wa magari mara baada ya kuruhusiwa kupita katika barabara ya juu katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akikagua barabara ya juu katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela kabla ya kuruhusu magari kuanza kupita eneo hilo katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo aliporuhusu magari kuanza kupita katika barabara ya juu eneo la makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa magari mara baada ya kuruhusiwa kupita katika barabara ya juu katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

Meneja wa barabara ya magari yaendayo haraka (BRT), Eng. Barakael Mmari akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipokagua na kuruhusu magari kupita juu ya barabara hiyo katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akiteta jambo na Mbunge wa Mbagala Mh. Abdalah Chaurembo alipokagua barabara ya juu katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa magari mara baada ya kuruhusiwa kupita katika barabara ya juu katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa barabara ya juu katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameruhusu magari kuanza kupita juu katika makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela jijini Dar es Salaam ili kupunguza msongamano kwa watumiaji wa barabara hizo.

Akizungumza alipokagua na kuruhusu magari kuanza kupita katika barabara hiyo, Prof. Mbarawa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha inapunguza  msongamano jijini Dar es Salaam na kuwawezesha wananchi kusafiri kwa uhakika na wakati.

“…TANROADS hakikisheni magari yanatumia barabara za juu kuanzia leo ili kumuwezesha mkandarasi kuendelea kujenga barabara za chini,” amesisitiza Prof.  Mbarawa.

Waziri huyo wa Ujenzi amesema kuanzia mwaka 2023 barabara inayoishia Mbagala itaendelea kujengwa kuanzia Mbagala hadi Vikindu KM 17 ili kupunguza kabisa msongamano katika barabara hiyo ya Kilwa.

Amemtaka Mkandarasi BOTEX anayejenga sehemu ya katikati ya Jiji kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha haraka eneo hilo na kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hizo.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka, BRT, Eng. Barakael Mmari amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa kazi ya ujenzi wa barabara hizo itakamilika kama ilivyopangwa  mwezi Machi mwakani na ujenzi kwa sasa umefikia asilimia 82. 

Naye Mbunge wa Mbagala Mhe. Abdallah Chaurembo amesema ujenzi wa barabara hiyo utapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Mbagala iliyokuwepo kwa zaidi ya miaka 15.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.


No comments:

Post a Comment