SERA YA UBIA YA NHC KUNUFAISHA TAIFA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 12 November 2022

SERA YA UBIA YA NHC KUNUFAISHA TAIFA

 

Meneja Habari na Uhusiano wa NHC Muungano Saguya, akizungumza na Waandishi wa Habari pembeni YAKE ni Meneja Masoko wa NHC, Julieth Buberwa.


Meneja Habari na Uhusiano wa NHC Muungano Saguya katika picha akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kusongezwa mbele kwa Uzinduzi wa Sera ya Ubia.

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limesema  Uzinduzi wa Sera ya Ubia, utafungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya nyumba na kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na uboreshaji wa majengo yanayomilikiwa na shirika hilo.

Uzinduzi wa Sera hiyo unatarajia kufanyika Novemba 16 mwaka huu, ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi.

Meneja Habari na Uhusiano wa NHC, Muungano Saguya amewaambia waandishi wa Habari kumekuwa na mwitiko mkubwa wa Washiriki ambapo jumla ya Washiriki 1000 kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, Vyama na Bodi za Kitaaluma na Wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki.

Saguya amesema pia Balozi zaidi ya 20, Taasisi za Kimataifa 10, Kamati ya Bunge ya Aridhi, Maliasili na Utalii na Wenyeviti wa Kamati za Bunge wamethibitisha kushiriki kwenye Uzinduzi huo.

Saguya alisema kumekuwa na utayari wa makampuni, Taasisi binafsi za nje na ndani kutaka kuwekeza katika ujenzi wa majengo na Viwanja vya NHC, hivyo Shirika limeona ni vyema kuchambua na kuainisha zaidi maeneo yatakayokidhi shauku ya Wawekezaji kinyume na maeneo yaliyotengwa awali.

Alisema awali yalitengwa maeneo 60 yenye Viwanja na Majengo yanayohitaji kuendelezwa na kwamba kutokana na msukumo wa Wawekezaji wamelazimika kuongeza maeneo kuliko pelekea kusongezwa kwa tarehe ya Uzinduzi.

Sera hiyo ya Ubia ilianzishwa na NHC tangu mwaka 1993 na kufanyiwa maboresho kadhaa kulingana na wakati husika ambapo maboresho ya mwisho yalifanyika mwaka 2022 kwa kuondoa changamoto zilizojitokeza hapa awali.

No comments:

Post a Comment