 |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye akiwa na wataalam wa wizara na TAWAH wakizindua rasmi Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam. |
 |
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam.
|
 |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye akifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam. |
 |
| Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wasanifu Majengo Tanzania (TAWAH), Arch. Siti Sheuya akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam. |
 |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye (kulia) akiteta jambo na Mwenykiti wa Bodi ya TAWAH, Bi. Winnie Terry kwenye hafla ya ufunguzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam. |
 |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye akimkabidhi zawadi mmoja wa wawezeshaji wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi, Mkadiriaji Majenzi, Neema Kadori. |
 |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye akiwa na wataalam mbalimbali wa wizara hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam. |
 |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam. |
 |
| Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi jijini Dar es Salaam. |
 |
| Mmoja wa wawezeshaji wa Programu ya kuwawezesha wanawake wataalam wa masuala ya Ujenzi, Mkadiriaji Majenzi, Neema Kadori akizungumza kwenye hafla hiyo. |
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya
Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye amesema Serikali itaendelea kushirikiana na
taasisi mbalimbali zenye lengo la kuwajengea uwezo wakadiriaji majenzi,
wasanifu majengo na wahandisi wanawake ili kuwa nasifa za kuajiriwa, kujiajiri
na kuajiri wengine.
Akizungumza katika hafla ya
ufunguzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake katika masuala ya ujenzi
iliyoandaliwa na taasisi ya wasanifu majengo Tanzania, (TAWAH) jijini Dar es
Salaam amezungumzia umuhimu wataalam hao kufanya mazoezi ya vitendo kwa wingi
ili kuwa na ujuzi na hivyo kuwawezesha wanawake kushiriki katika maendeleo ya
sekta ya ujenzi nchini.
"...Serikali inatenga asilimia
30 ya Bajeti ya Ujenzi wa Barabara kwa ajili ya miradi inayotekelezwa na
wanawake hivyo waongezeeni ujuzi ili waweze kunufaika na fursa hiyo,"
amesema Naibu Katibu Mkuu Nduhiye.
Nduhiye amezungumzia umuhimu wa
wataalam wa ujenzi wanawake kuunda vikundi kufungua kamapuni na kuoba kazi za
ujenzi na Serikali itawaunga mkono katika hatua zote.
Kwa upande wake, Mdhibiti ubora wa
Bidhaa za Kampuni ya Saruji ya Tanga, Bw. Shukrani Chindoli amewataka waalam wa
ujenzi kuzingatia usalama wakati wote ili kufanya sekta ya uje kuwa mahali
salama pa watu kufana kazi.
Naye Msajili wa Bodi ya Wasanifu
Majengo na Wakadiriaji Majenzi Arch. Edwin Nunduma ameipongeza TAWAH kwa
jitihada inazofanya kuwawezesha wataalam wa ujenzi wanawake na kuahidi
kushirikiana nayo ili wataalam hao wasajiliwe na kuwa na sifa za kufanya kazi
ndani na nje.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake
Wasanifu Majengo Tanzania (TAWAH), Arch. Siti Sheuya ameishukuru Serikali kwa
jitihada inazozifanya kuwawezesha wataalam wa ujenzi wanawake na kuahidi kuwa
watazingatia uzalend, uadilifu na kufanya kazi kwa bidiii.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment