Mada zikiendelea kutolewa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Na Mwandishi Wetu, Same Kilimanjaro.
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo amefungua
Kongomano la kumbukizi ya miaka 23 tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalim
Julius Nyerere ambalo pamoja na mambo mengine limejadili maono mbalimbali
ambayo baba wa taifa aliyoyafanya enzi za uhai wake.
Mpogoro wakati akifungua kongamano hilo ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa
kina jitihada ambazo zilifanywa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake
kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja na kudumisha mshikamano huku
akipenda kuona watu wake wanapiga hatua kimaendeleo.Askofu Mstaafu wa Kanisa
Katoliki, Jacob Koda ameiomba Serikali kufufua Viwanda vyote vilivyokuwa
vikifanya uzalishaji enzi za Mwalimu Nyerere ikiwa kama njia mojawapo ya
kumuenzi Mwalimu.
Kwa upande wake Askofu Koda aliyasema hayo wakati akitoa mada kuhusu
Mchango wa Mwalimu katika kukuza uchumi na Maendeleo endelevu ambapo alisema
Nyerere alijitahidi kuanzisha viwanda katika mikoa mbalimbali ili kukuza
uchumi.
Alisema Baba wa Taifa alitambua ili nchi iweze kuwa na Maendeleo endelevu
lazima kuwe na viwanda na ndipo alipoanzisha viwanda vya nguo kwenye mikoa
karibu yote, kulikuwepo na viwanda vya ngozi vikitengeneza
viatu, mabegi, kulikuwepo na viwanda vya magunia na kiwanda Cha General Tyre cha
Arusha ambacho kilikuwa kinaaaminika kwa matairi bora Afrika Mashariki.
Wakati huo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo aliahidi kuuchukua ushauri wa Askofu na kuufanyia kazi.
Katika kongamano hilo mada mbalimbali zilitolewa na watoa mada wabobezi waliopata bahati ya kumjua Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
No comments:
Post a Comment