RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Alhaj, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea jengo jipya la ofisi pamoja na ukumbi wa mikutano katika Msikiti Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wa Mohamed wa Sita Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam na kufurahishwa na ubora na miundombinu yake ya kisasa.
Alhaj Dkt. Kikwete, aliyeongozana na mkewe Mbunge wa Mchinga Mhe. Hajjat Salma Kikwete, ametembelea jengo hilo mara baada ya kuhudhuria Swala ya Ijumaa katika msikikti huo mkubwa uliojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco.
Akawashauri BAKWATA kuwa wasifanye ajizi katika kuutunza na kuuweka katika mazingira ya usafi msikiti huo na majengo yake ili uendelee kutoa huduma bora kwa waumini katika swala na shughuli mbalimbali za kidini na kijamii kama ulivyokusudiwa.
Akiwa anatembezwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaj Nuhu Jabir Mruma Dkt. Kikwete alitembelea ukumbi wa mikutano wa kisasa pamoja na maktaba ya historia iliyosheheni maandishi ya awali ya Quran Tukufu yaliyoandikwa kwa mikono na wanazuoni wa kale.
No comments:
Post a Comment