![]() |
| Mkurugenzi wa (HLI) Kanda ya Afrika Mashariki kwa Nchi zinazozungumza Lugha ya Kingereza Emil Hagamu na kulia ni Padri Dennis Ombeni Mkurugenzi wa Idara ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Jimbo Kuu Katoliki Arusha. |
Na Frida Manga, Arusha
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Mhashamu Isack Amani, amesema Muswada wa Ujinsia na Afya ya Kizazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 2021 haufai kwa maisha ya mwanadamu na hivyo unapaswa kupingwa kwa nguvu zote.
Ni katika mkutano wa kupinga kupitishwa mswada huo uliondaliwa na Shirika la Kimataifa la Kutetea Uhai Kanda ya Afrika (Human Life International) na kufanyika jijini Arusha.
Askofu Amani akatumia wasaa kuwahasa Wabunge wa Bunge wa Jumiya ya Afrika Mashariki (East African Legislative Assembly - EALA) kuhakikisha kwamba wanalinda Uhai wa Raia wa Nchi hizo, kulinda tamaduni zake na utu wa Raia wake na kuwaepusha na uovu ambao unakwenda kinyume na mpango wa Mungu kwa mwanadamu lakini pia unaokwenda kinyume na tamaduni za watu wa Arika Mashariki.
Pia amewataka viongozi na wawakilishi hao wa wananchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EALA) kutambua kwamba wanaowajibu mbele ya Mungu na wanadamu kulinda uhai wa raia wa nchi za Jumuiya hiyo na kuwaepusha na mambo maovu, na kwamba si kila kitu kinacholewata kwao kinapaswa kutumika na badala yake wanapaswa kuchambua kwanza na kjiridhisha ikiwa kuna faida kwa watu.
Mswada huo unatajwa kuwa na vipengele ambavyo ni viovu na ambavyo vinakiuka utu wa uhai wa Watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia unakwenda kinyume na tamaduni za watu ambao pia unataka kuwaingiza watu katika utamaduni wa kifo.
Askofu Amani alisema ni marufuku wanadamu kucheza na uhai wa mwanadamu tangu kutungwa mimba hadi kifo chake cha kawaida kwani uhai ni kitu kitakatifu ulioumbwa na Mungu mwenywe hivyo kinapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa na kila mtu.
”Alisema neno la Mungu linafundisha kwamba uhai ni kiitu kitakatifu kinachotoka kwa Mungu, ambao umeumbwa na Mungu mwenyewe, na kwamba mwanadamu mwenye akili timamu anapaswa kushiriki katika kuthamini uhai wa mwanadamu mwingine,” Alisema Askofu Mkuu Amani.
Miongoni mwa vipengele hivyo ni kipengele kinachotaka ama kinacholazimisha nchi za Afrika Mashariki kufanya matumizi ya vithibiti mimba kuwa sehemu ya maisha yao bila kujali umri, wala hali ya ndoa na hasa kulazimisha matumizi yake kwa watoto.
Hali kadhalika kipengele kinachotaka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunga Sheria za kutoa mimba amabyo kama itapitishwa kuwa sheria, wananchi wa Jumuia ya Afrika Mashariki watakuwa wameanza mradi wa kuangamiza kizazi cha baadaye.
Pia kipengele kinacholazimisha masomo ya ngono ambayo yanaharibu ukuwaji wa watoto na kuleta mmomonyoko wa maadili. Kipengele kingine kibaya ni kile cha kuingilia kati uumbaji wa binadamu kwa kuhamasisha matumizi ya tekenolojia saidizi ili kupata uzao.
Mkurugenzi wa (HLI) Kanda ya Afrika Mashariki kwa Nchi zinazozungumza Lugha ya Kingereza Emil Hagamu alisema walipata taarifa miezi mingi iliyopita juu ya Muswaada huo na kuchukua hatua mbalimbali na walipousoma wabaini kwamba ikiwa utapita utaharibu na kuleta madhara kwa watu wa nchi za Afrika Mashariki.
Hagamu alisema mbaya zaidi ni kwamba mswaada huo umeegemea kifungu ambacho si sahihi kifungu cha 118 cha Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mshariki kinachohusu maswala ya Afya.
Kwa mujibu wa Hagamu ikiwa Muswaada huo utapita utaathiri maisha ya watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo ni vyema ukatupiliwa mbali kwani hauna manufaa yeyote na ikiwa kuna ulazima kwa kandikwa mswaada basi uandikwe mwingine wenye tija kwa raia wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa (HLI) Uganda Padri Jonathan Opio aliwataka washiriki wa Mkutano huo kusimama imara bila kuchoka na kupaza sauti zao katika kupinga mswaada huo unamadhara makubwa kwa uhai wa mwanadamu.
Betty Sammaaye ni Mshiriki katika katika Mkutano huo, ambapo amewataka wazazi kuzungumza na watoto wao, kuwaeleza ukweli kila kinachoendelea kuhusu maisha yao ya baadaye ambayo yamegusiwa na katika mswada huo.
Kupitia Mkutano Washiriki wakatoa maazimio yao kama raia wa Tanzania lakini pia kama Wazazi, ambapo taamko la maazimio hayo lilisomwa na Padri Dennis Ombeni ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulinzi na Usalama wa MTOTO Jimbo Kuu Katoliki la Arusha.
Washiriki hao wamekubalina kwa pamoja kwamba wanaukataa Muswaada huo wenye kushinikiza mawazo ya ukoloni mamboleo kwa ujumla wake, kwamba wamekataa majaribio ya kushashadia uzuri usio kuwa na tija kwa na hatima nzuri kwa watoto wao.
Pia wamekataa na kulaanini hatua na juhudi zinazofanywa za kunyanyasa watoto kwa njia ya ngono na unyonyoji wa kiuchumi kupitia uhalalishaji wa matumizi ya vithibiti mimba na utoaji wa mimba, pia kukataa kudhalilishwa na kudharauliwa kwa tamaduni za watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Na mwisho azimio hilo limewataka wabunge wa Bunge la EALA, kuzingatia ujenzi wa Nchi wanachama kama ilivyofafanuliwa kwenye Mkataba uliounda Jumuiya hiyo kwa ustawi kwa Nchi wanachama na wananchi wake.




No comments:
Post a Comment