AKIBA COMMERCIAL BANK YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZAKE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 19 August 2022

AKIBA COMMERCIAL BANK YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZAKE

 Meneja Mwandamizi wa idara ya Biashara, Bw. Emmanuel Mseti.

Na Mwandishi wetu.


BENKI
ya Biashara ya Akiba (ACB) katika kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake inafanya jitihada kuboresha huduma na bidhaa mbali mbali kuendana na mahitaji ya wateja na soko kwa ujumla.

Hivi karibuni Meneja Mwandamizi wa idara ya Biashara, Bw. Emmanuel Mseti katika mahojiano na vyombo vya habari amesema kuwa Benki ya Akiba imefanya maboresho kwenye utoaji huduma kwa wateja wake.

Akifafanua katika mahojiano , Bw.Mseti alisema kuwa huduma zao zimeboreshwa katika nyanja mbalimbali hasa upande wa wateja binafsi.

“Huduma hizi tumeziboresha kwenye akaunti ya mishahara (Akiba Salary Account). Mteja ambae yuko Akiba au mteja mtarajiwa anaweza kunufaika kwa kupata kupata huduma mbali mbali zilizounganishwa na akaunti hii mathalan; mikopo ya wafanyakazi, mikopo ya nyumba pamoja na ‘Salary Advance’ kwa ajili ya dharura na fursa zinazojitokeza papo kwa papo.” Huduma hii inaptikana ndani ya mfupi iwezekanavyo kufutia uharaka wa mteja katika kufanikisha taratibu zinazohitajika. Huduma hii inaweza kupatikana ndani ya masaa 24. nyongeza ya mshahara, kupokea mshahara kila mwezi na kuweka akiba ya pesa zake” Alisema. 

Aliongeza kuwa, muda wa marejesho wa mikopo ya nyumba umeongezwa kufikia miezi 84 au miaka 7 kwa ajili ya kuleta unafuu kwa mkopaji katika kumudu marejesho. Vile vile mikopo hiyo ya nyumba ijulikanayo kama Akiba Mortgage loan inatolewa kwa ajili ya kununua nyumba, kujenga nyumba, kumalizia ujenzi pamoja na kufanya marekebisho (renovation).

Aidha, Bw. Mseti alisema, Benki ya Akiba pia inatoa huduma ya mikopo inayodhaminiwa na hati fungani za Serikali (Loans backed by Government Bonds) kwa watu walioajiriwa na wasioajiriwa, hati fungani itasimama kama dhamana ya kupata mkopo. Mbali na hivyo Mseti pia alisema Akiba Salary ina gharama nafuu za uendeshaji na akunti hii pia imeunganishwa na huduma za kidijitali kama Akiba mobile zinazoleta urahisi zaidi kwa mteja katika kupata mahitaji ya kibenki.

Akiba Commercial bank inaendelea kuboresha huduma zake pamoja na kuanzisha nyingine nyingi mpya ili iweze kuwahudumia Watanzania wote na wafanya biasharab kuanzia wa tabaka la chini, kati na wa juu hususan makampuni makubwa na taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mseti , mbali ya kuwa na matawi sehemu mbali mbali Benki pia imefanikiwa kuwa na mawakala zaidi ya 1500 nchi nzima kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wao .

No comments:

Post a Comment